Usalama wakwamisha wakimbizi DRC kurudi kwao

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limesema kuwa wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wanaohifadhiwa kwenye kambi ya Nyarugusu wilayani ya Kasulu mkoani Kigoma hawataweza kurudishwa nchini kwao kwa sasa kutokana na maeneo wanayotoka kuwa na hali mbaya  ya usalama.

Mwakilishi mkazi wa UNHCR nchini, Barbara Bentum Dotse  akizungumza kwenye mkutano na wakimbizi wa DRC kwenye kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Kasulu alisema kuwa shirika hilo haliko tayari kuwarudisha wakimbizi hao kutokana na hali mbaya ya usalama iliyopo kwenye maeneo hayo ambapo vita ya wenyewe kwa wenyewe inaendelea

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa UNHCR itaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuwahudumia wakimbizi hao hivyo limetoa wito kwa wakimbizi hao kuishi kwa kufuata sheria na taratibu za kuishi kambini hapo zilizowekwa ili kuepuka kuvunja sheria.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi ya Wizara ya Mambo ya Mdani ya Nchi, Sudi Mwakibasi alisema kuwa kutoweka kwa amani katika maeneo yao kutokana na migogoro ya kijamii na kisiasa ndiyo iliyowafanya wakimbizi hao kukimbia nchi yao na kukimbilia nchini na hali hiyo bado inaendelea hivyo wakimbizi hao hawataweza kurudishwa kwao katika hali hiyo.

Aidha, mkurugenzi huyo wa idara ya wakimbizi amewataka wakimbizi hao wa DRC kuishi kambini humo kwa kuzungumzia masuala yanayohusu amani badala ya mambo yanayowapelekea kuvunja sheria na kwamba Amani itakaporejea taratibu za kuwarudisha nchini kwao zitatekelezwa.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I’m making over $25,000 a month working part-time. I kept hearing other people talk about how much money they were making online, so I decided to look into it. Well, it’s all true and has completely changed my life. This is what I do. Check it out by visiting the following link:

    COPY THIS →→→→ http://Www.Work99.Site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button