Ushahidi kesi ya uhaini ya Lissu kuanza leo

MAHAKAMA Kuu Masijala Ndogo Dar es Salaam leo inatarajiwa kuanza kusikiliza ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

Kwa mujibu wa Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga katika kikao cha mahakama kilichopita, upande wa Jamhuri unatarajiwa kuwa na mashahidi 30 na idadi kadhaa ya vielelezo wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo Mahakama Kuu ili kuthibitisha hatia ya mshitakiwa na Lissu anatarajia kuwa na mashahidi 15 katika utetezi wake.

Shauri hilo litasikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru akisaidiana na Jaji James Karayemaha na Jaji Ferdinand Kiwonde.

Katika usikilizwaji wa shauri hilo, mahakama hiyo imesisitiza itaendelea kusimamia uamuzi wa mahakama uliotolewa wakati shauri likiwa katika mahakama ya ukabidhi ya kulinda mashahidi kwa kutokurusha matangazo mbashara wakati wa usikilizwaji kwani inaweza kuathiri ulinzi wa mashahidi pamoja na ushahidi wao.

Pia, ikisisitiza hakuna sababu ya kufanya hivyo kwani mahakama hiyo itaendesha shauri hilo kwa uwazi kwa kuruhusu waandishi wa habari kuripoti kwa namna inayofaa, pia kuepusha mashahidi kuiga maelezo ya mashahidi wengine.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, ilidaiwa Aprili 3, 2025 jijini Dar es salaam mshitakiwa Lissu akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitengeneza nia ya kushawishi au kuchochea umma kuweza kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kwa kusema maneno yafuatayo;

“Walisema msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi tutahamasisha uasi, hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko… kwa hiyo tunaenda kukinukisha sanasana huu uchaguzi, tutaenda kulivuruga kwelikweli, tunaenda kukinukisha vibaya sana”.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button