Ushirikiano wahitajika kutatua changamoto Ukerewe

MWANZA; MKUU wa Mkoa wa Mwanza, CP Salum Hamduni, amewataka wananchi wa Wilaya ya Ukerewe kushirikiana na Serikali katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili, ikiwemo upatikanaji wa maji, umeme na barabara.

CP Hamduni ametoa kauli hiyo leo Septemba 22, wakati akizungumza na wananchi wa Ukerewe, ambapo amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wananchi, watumishi wa umma na taasisi za Serikali katika kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utatuzi wa kero.

Amesema changamoto ya maji na umeme ni miongoni mwa kero zinazohitaji ushirikiano wa pamoja ili kupata ufumbuzi wa kudumu, huku akiwataka wananchi kumpa muda wa kushughulikia changamoto hizo.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka watumishi wa umma na taasisi za Serikali zilizopo Wilaya ya Ukerewe kutoa huduma kwa wananchi kwa usawa, haki na kwa wakati, bila kujali hadhi ya mtu.

“Tabia ya kusubiri viongozi tufike ndiyo tutatue kero sio sawa. Watumishi wa umma watoe huduma kwa ubora na wakati bila kuangalia hadhi ya mtu,” amesema CP Hamduni.

Amesisitiza kuwa huduma za Serikali zinapaswa kutolewa kwa wakati ili wananchi wasilazimike kusubiri viongozi wa kisiasa au Serikali kufika maeneo yao ndipo changamoto zianze kushughulikiwa.

CP Hamduni pia amewataka wakazi wa Ukerewe kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali na kumpa muda wa kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.

Kwa upande wake, Mariam Chiluma, mkazi wa Nansio, amesema wananchi wanakabiliwa na changamoto za maji, barabara na umeme, akieleza kuwa kero hizo zinahitaji hatua za haraka ili kuboresha maisha ya wananchi.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button