Uwanja wa ndege Ibadakuli kukabidhiwa April Mosi 2025

WAKALA ya Barabara (TANROADS) mkoani Shinyanga umesema utakabidhi Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli uliopo Manispaa ya Shinyanga ifikapo April Mosi, 2025.

Msimamizi Mwakilishi wa Tanroads, Mhandisi Chiyando Matoke amesema hayo leo mbele ya waandishi wa habari alipotembelea uwanja huo Shinyanga.

Mhandisi Matoke amesema uwanja huo ulitakiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka 2024 kutokana na kuongezeka maeneo ya kufanya kazi kama ongezeko la njia ya kupitia ndege, kipande cha barabara ya lami, uzio na miundombinu ya zimamoto ndiyo vimeongeza muda wa kazi.

Advertisement

“Gharama ya ujenzi wa uwanja huo ni Sh bilioni 44.8 bila VAT ujenzi huo ulianza mwaka 2023 hadi mwaka 2025 ambapo uwanja huo umepanuliwa kwa kilomita 2.2 na urefu wa hifadhi ya barabara mita 30,”amesema Mhandisi Matoke.
Msimamizi wa mradi huo Mhandisi Kahatona Ruburi amesema uwanja huo unaitwa 1129 unaweza kutua ndege nne ambapo kubwa mbili na ndogo mbili na mradi umehusisha ujenzi wa uzio, mtaro na uwanja wenyewe.
Mhandisi Msimamizi wa mradi huo upande wa jengo Fatuma Mruma amesema jengo la wasafiri limefikia asilimia 50 na likikamilila linatarajia kuchukua abiria 200.

Msimamizi usalama wa uwanja huo Geremiah Kileo amesema ndege zimeanza kuruka muda wa mchana kwa kuwatumia wataalamu wa hali ya Mamlaka ya hewa kutoka Mwanza na Tabora nakupeana hali ya usalama.