Uwepo wa SGR uhakika wa umeme
DODOMA : NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Doto Biteko amesema safari za treni za reli ya kisasa (SGR) zinazotumia umeme kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ni ushahidi kuwa Tanzania ina umeme wa kutosha.
SOMA : Waziri Mkuu atoa maelekezo uendeshaji SGR
Dk. Biteko ameyasema hayo leo Septemba 12, 2024 baada ya kuwasili jijini Dodoma akitokea Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa treni ya mwendo kasi (SGR) kwa mara ya kwanza