Uzalishaji nyama waongezeka

UZALISHAJI wa nyama umeongezeka kwa asilimia 4.3 kutoka tani 769,966.7 mwaka 2021/2022 hadi tani 803,264.3 mwaka 2022/2023.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024.

“Kati ya hizo, tani 544,983.8 ni za nyama ya ng’ombe; tani 113,781.8 za nyama ya mbuzi na kondoo; tani 96,915.6 za nyama ya kuku na tani 47,583.1 za nyama ya nguruwe.

“Ongezeko hilo limechangiwa na wafugaji kuhamasika kuvuna mifugo yao na kukua kwa soko la nyama la ndani na nje ya nchi.

“Aidha, uzalishaji wa nyama ya ng’ombe uliongoza, ukifuatiwa na nyama ya mbuzi na kondoo, kuku na nguruwe,” amesema Waziri Ulega.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x