Uzoefu kuivusha salama Tanzania Uchaguzi Mkuu 2025

UZOEFU mkubwa ambao Tanzania imeupata katika kuandaa na kufanikisha chaguzi sita kwa amani na utulivu umetajwa kuwa ni kete muhimu ya kuivusha nchi salama katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Wadau na wafuatiliaji wa uchaguzi wanasema ushahidi wa hoja hiyo unaonekana kwenye uzinduzi wa kampeni ulioanza wiki iliyopita ambao umefanyika kwa amani, utulivu na usalama hali inayotoa taswira nzima ya kampeni za mwaka huu.
Tanzania, tangu kupata uhuru wake imekuwa ikitajwa kama kisiwa cha amani huku ikitumiwa kama darasa la utulivu na amani na nchi nyingine duniani, sifa ambayo imetengenezwa na waasisi wa taifa hili na ambayo inapaswa kuendelea kuenziwa kwa kuhakikisha hakuna upenyo wa kuivuruga amani kwa namna yoyote.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na mchambuzi wa masuala ya siasa, Dk Paul Loisulie anasema Tanzania imeshapata uzoefu wa kutosha kupitia chaguzi sita zilizopita na hakuna anayetarajia kama kuna kitu cha ajabu kitakachotokea katika uchaguzi wa mwaka huu. “Itakuwa ajabu kwamba baada ya kuwa tumeshapata uzoefu ndiyo tunakuja kufanya kitu cha kuharibu uchaguzi na kuiharibu nchi yetu,” anasema.
Anasema uchaguzi unaendeshwa kwa taratibu, sheria, kanuni na miongozo ambayo imetolewa na mamlaka inayotambulika na kwamba vyama havina budi kuzingatia taratibu hizo kwa sababu vikienda kinyume kunaweza kutokea uvunjifu wa amani. “Vyama pia, wajue kuna maisha baada ya uchaguzi wasije wakafanya vitu kwa kupitiliza wakati mwingine kuna hamasa au mihemko iliyopitiliza vyama viepuke mihemko.
Wasiwashawishi wafuasi wao kufanya kitu ambacho kinaweza kuharibu amani,” anasema. Dk Loisulie anasema kipindi cha uchaguzi kitaisha na maisha mengine yatapaswa kuendelea hivyo amani ni jambo la msingi. SOMA:
Anasema wakati wa uchaguzi wagombea wanapaswa kuzingatia sheria na kuuza sera zao na siyo kufanya kampeni kwa kuzungumza mambo madogo ikiwemo kuzungumzia watu, badala yake wajikite katika kueleza watakayoyafanya iwapo watachaguliwa.
“Kampeni ijikite kwenye masuala ya kiuchumi ya kijamii na mengine isihusu mambo mengine ambayo hayafai, pia wagombea wajaribu kuwahimiza wafuasi wao kwani wagombea ndio kwa kiasi kikubwa wameshikilia ile kampeni kwa sababu wanaaminika, wanasikilizwa, kwa hiyo wasitamke kitu ambacho kitawafanya wafuasi waje wafarakane,” anasema.
Wananchi nao wanalo jukumu wakati kampeni zinapoendelea, Dk Loisulie anasema wanapaswa kuwasikiliza wagombea na kufanya maamuzi lakini wasikubali kuingia kwenye mtego wa mafarakano. “Wananchi wakati mwingine wanalazimisha mahaba kiasi kwamba wanafanya vitu kwa mihemuko kwa hiyo tujue tu kwamba wagombea wapo tuwasikilize halafu tuamue tusikubali kuingia kwenye mifarakano, kwenye fujo kwa sababu mwisho wa siku sisi wenyewe wananchi ndio tutakaoumia. Tuwape nafasi tuwasikilize halafu tufanye maamuzi,” ameongeza.
Mtaalamu wa siasa na mdau wa masuala ya uchaguzi, Dk Albanie Marcossy anasema kampeni ni mchakato unaohusisha kupashana habari ili wananchi waweze kufanya maamuzi. Anaongeza kuwa wapigakura wana nafasi ya kuwaambia wagombea na vyama vya siasa vitu wanavyovihitaji na wasivyovipenda na vyama vya siasa kukusanya taarifa kutoka kwa wananchi juu ya mambo hayo.
“Wapigakura nao huwa wana nafasi ya kuwaambia wagombea na vyama vya siasa vitu gani wanavipenda vipi hawavipendi, kwa hiyo jukumu la kwanza la vyama vya siasa ni kuhakikisha wanakusanya taarifa kutoka kwa wananchi iwezekanavyo juu ya vitu wanavyovipenda na wasivyovipenda,” anasisitiza. SOMA: Wagombea, vyama vizingatie kampeni za kistaarabu kulinda amani ya nchi
Anasema wanapaswa kuwasikiliza wagombea na vyama vyao na kuchambua mambo gani wanayotaka yafanyike na namna ambavyo wagombea wamejipanga kuyatekeleza. Anasema jambo jingine ambalo wapigakura wanatakiwa kufanya ni kufanya uchambuzi na tathmini ya ahadi zilizowahi kutolewa na wagombea wanaotetea nafasi zao, iwapo wamezitekeleza kwa ukamilifu na kama hazikutelezwa ni kwanini ili waweze kufanya uamuzi sahihi kupitia kura zao.
“Na wao wagombea wanatakiwa kueleza vitu wanavyotarajia kuvifanya viwe miongoni mwa vile ambavyo wanavitarajia (wananchi) na vingine hata ambavyo hawajavitarajia lakini wao wanaona vina maslahi kwa umma, kuhakikisha taarifa hizo zinawafikia vizuri ikiwa ni pamoja na kuepukana na upotoshaji,” anasema.
Anasema jukumu jingine la wagombea ni kuwaondolea wananchi hofu juu ya usalama wa nchi wakati wa kampeni na mchakato wote wa uchaguzi. Wakati wa mahojiano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) hivi karibuni, Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye anatoa wito kwa Watanzania wote wakiwemo viongozi wa kisiasa, kuepuka kufanya vitendo vyovyote vinavyoweza kuathiri amani na utulivu wa nchi, hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Sumaye anasisitiza kwamba ni muhimu kwa Watanzania kudumisha umoja ili kuendelea kuiwezesha Tanzania kuwa taifa linaloenzi utu, haki, amani na utulivu. “Mimi nataka niwaombe Watanzania, siasa ipo tu siku zote, hata kama hujaridhika bado kwenye siasa tunasema tunajiandaa na kipindi kingine, tusifanye jambo lolote ambalo linaweza likaumiza amani, utulivu wetu na mshikamano wetu, bado tunajihitaji kama Taifa tuwe kitu kimoja,” anasema.
Anaongeza: “Mambo hayo kwamba leo umekosa hapa kesho pale unadhani umeonewa na nini yanazungumzika, tuyarekebishe kwa utulivu na amani, tusifanye fujo hata kidogo! Uchaguzi huu upite kwa utulivu na kwa amani, Tanzania tuendelee kuwa na sifa yetu ya kuwa taifa ambalo linajali utu haki amani na utulivu.”
Anasema zipo nchi nyingi ambazo zimeharibu amani na utulivu wao sasa na kwamba Watanzania hawatakiwi kuiga huko, kwani kama Watanzania kuna utaratibu, kawaida na mshikamano baina yao, hivyo ni vyema kuendelea kuwa kitu kimoja. “Siasa tutaikuta tutairekebisha palipo na tatizo ili tuendelee kuwa nchi inayoheshimika na sisi wenyewe tunajiheshimu, bila amani na utulivu tukubali kwamba hakuna maendeleo,” anasisitiza Sumaye
PATA HABARI YA WWE MILIKI KIWANJA CHA KIWANDA PAMOJA NA £56,565,656,000 ONLINE LIVE HAPA + UCHAGUZI UKIISHA UTAGAWA KWA WATANZANIA £56,565,656,000 /56,000,000 maana tumekukabidhi NYOTA Yetu YA KUPATA HELA
PAMOJA NA bonanza la “We JuDGE….”
https://youtube.com/shorts/_jB1m_sfFuM?si=wSugXDCDnASW1bK6
Everybody can earn 220$/h + daily 1K… You can earn from 6000-12000 a month or even more if you work as a part time Work…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good eaning opportunity..go to this site home tab for more detail thank you…….
.
Reading This Article:———————- http://Www.Cash43.Com
PATA HABARI YA WWE MILIKI KIWANJA CHA KIWANDA PAMOJA NA £56,565,656,000 ONLINE LIVE HAPA + UCHAGUZI UKIISHA UTAGAWA KWA WATANZANIA £56,565,656,000 /56,000,000 maana tumekukabidhi NYOTA Yetu YA KUPATA HELA
PAMOJA NA bonanza la “We JuDGE….”
https://youtube.com/shorts/_jB1m_sfFuM?si=wSugXDCDnASW1bK6
I just got paid $22k working off my laptop this month!** And if you think that’s cool, my divorced friend has twin toddlers and made over $22620 her first month. details on this website**Want the secret?** Copy this Website and choose HOME TECH OR MEDIA…..
Here is I started_______ https://Www.CashHive1.Com