Vifo vitokanavyo na ajali migodini vyapungua

IDADI ya vifo vitokanavyo na ajali katika maeneo ya migodi vimepungua kwa kiasi kikubwa kutoka 106  ilivy ripotiwa mwaka 2018 hadi kufikia 33 mwaka 2022.

Katibu Mtendaji Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, alisema kwenye kikao kazi cha wakaguzi wa migodi na baruti nchini kilichofanyika jana mkoani Morogoro.

Mhandisi Samamba alisema licha ya idadi ya vifo kupungua, pia idadi ya matukio ya ajali ya watu walizopata ulemavu, navyo vimepungua kutoka 43 hadi kufikia 16.

“Hapo nyuma matukio ya ajali migodini yalikuwa kwa wingi sana, tumefanya kazi kubwa, ili kuhakikisha matukuo ya ajali na vifo vinapungua,”alisema Yahya.

Alisema matukio  ya ajali migodini kwa wachimbaji wakubwa na wakati yamejitokeza kwa kiasi kidogo tofauti na wachimbaji wadogo, kwani ndiyo waathirika  wakubwa wa ajali hizo na hiyo ni kwa sababu na uduni wa teknolojia wanazozitumia.

Katibu  Mtendaji huyo  alimpongeza  Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira pamoja na wakaguzi wa tume hiyo kwa kitendo cha kuchukua hatua ambazo zimewezesha kusaidia kupunguza matukio ya ajali na vifo migodini.

Aliwataka wakaguzi wa migodi na baruti kutumia kikao kazi hicho kama fursa pindi watakaporudi katika maeneo yao ya kazi, kuwaelimisha wachimbaji katika suala zima la utunzaji wa mazingira, ili kuepukana na athari za  mabadiliko ya tabianchi.

Naye Mkaguzi Mkuu wa Migodi, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ukaguzi Migodi na Mazingira, Mhandisi Henry Nditi, alisema kuwa kikao kazi hizo  ni cha kuwajengea uwezo zaidi, ari na nguvu mpya kwa wakaguzi wa migodi katika kutekeleza majukumu yao.

Alisema  kuwa ili uchimbaji wa madini uwe endelevu lazima kuwe na  usalama, kusiwe na ajali na utunzaji wa  mazingira  kwa manufaa ya kizazi cha sasa na cha baadaye na ina umuhimu katika kukuza sekta ya madini nchini.

Habari Zifananazo

Back to top button