Vijana Dar wajifunza afya ya akili, uzazi

DAR ES SALAAM; Vijana zaidi ya 250 wamejifunza mada mbalimbali zinazohusu maisha yao zikiwemo afya ya akili, afya ya uzazi, kujitambua na umuhimu wa kushiriki katika kufanya maamuzi yanayohusu maisha yao.
Mafunzo hayo yalitolewa katika kongamano la nne la Young and Alive Summit lililofanyika kwa siku tatu jijini Dar es Salaam, likiwa na mijadala mbalimbali pamoja na utoaji wa huduma za afya kwa washiriki.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Young & Alive Initiative, Dk Cecilia Shirima, amesema kongamano hilo lililenga kuwajengea vijana uelewa kuhusu masuala yanayowahusu na kuwapa nafasi ya kubadilishana uzoefu kuhusu changamoto wanazokutana nazo katika jamii.
“Mijadala iliyofanyika ilijikita katika afya ya uzazi, afya ya akili na kujitambua, huku vijana wakijadili namna wanavyoweza kushirikiana katika kutatua changamoto na kuleta mabadiliko chanya katika maeneo yao,” amesema.
Dk Shirima amesema kongamano hilo pia lililenga kuimarisha ushirikiano miongoni mwa vijana kutoka mikoa mbalimbali ili waweze kuungana na kutumia nguvu zao katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili.
Amesema washiriki walipata fursa ya kuchambua sera na miongozo mbalimbali inayohusu vijana na kujadili namna wanavyoweza kuitumia katika majukumu yao ya kila siku.

Amesema kongamano hilo lilishirikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, viongozi vijana, wawakilishi wa mashirika ya vijana pamoja na wadau wanaofanya kazi katika masuala ya afya na ustawi wao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto ya Wizara ya Afya, Dk Mzee Nassoro, amesema kongamano hilo ni muhimu kwa kuwa linatoa nafasi ya kujadili mahitaji na changamoto za vijana nchini.
Dk Nassoro, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya katika kilele cha kongamano hilo, amesema vijana ni kundi muhimu linalopaswa kupewa kipaumbele katika mipango ya maendeleo na utoaji wa huduma za afya.
“Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi zinaonesha kuwa vijana ni zaidi ya asilimia 35 ya watu wote nchini, jambo linaloonesha umuhimu wa kuwekeza katika afya na ustawi wao,” amesema.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com