Vijana Mwanza wahamasishwa uchaguzi mkuu

MWANZA: VIJANA nchini wameshauriwa kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 ili waweze kupiga kura ikiwa ni sehemu ya kutimiza wajibu wao kikatiba.
Rai hiyo imetolewa leo na Waziri mstaafu Lazaro Nyalandu wakati wa mahojiano malumu na wandishi wa habari Mkoa wa Mwanza.

Nyalandu ameshauri vijana watumie fursa ya demokrasia ya Uhuru wa Tanzania kwa kupiga kura pamoja na kusaidia wazee wanapokuwa katika foleni ya upigaji kura.
“Nawaomba vijana kushawishiana kwenda kupiga kura na vijana wanapopiga kura ni jambo jema sana. Nawaomba vijana wajitaidi kutunza amani kwakuwa amani ukipoteza hairudi kirahisi. Amani ni tunu kubwa sana na tuilinde,” amesema.
Ameongeza kuwa tusiruhusu mtu yoyote avunje amani yetu. Amesema tofauti na vijana, naiomba jamii ya Kanda ya Ziwa kujitokeza vituoni kwenda kupiga kura.



