Vijana waanza kuikubali sekta ya kilimo

SERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na India imeanza kuchukua hatua za kuendeleza sekta ya kilimo kwa kuandaa majukwaa yanayowaunganisha wadau, kubadilishana maarifa na teknolojia pamoja na kuibua fursa za ubia wa kibiashara.

Mkurugenzi Mtendaji wa TAB Group, Tahir Bari, amesema hayo leo, Septemba 3, 2026, jijini Dar es Salaam wakati wa Maonesho ya 10 ya Kimataifa ya Kilimo Barani Afrika, yaliyoambatana na Maonesho ya Tatu ya Kilimo, Mifugo na Ufugaji wa Kuku.

Amesema amevutiwa na ushiriki mkubwa wa vijana katika maonesho hayo, akisema wengi wameanza kuiona kilimo kama biashara na wako tayari kujifunza na kutumia fursa zilizopo. Kufuatia matumizi ya teknolojia na mifumo ya kidijitali inaweza kuwawezesha vijana kuongeza tija hata katika mashamba madogo bila kuhitaji mtaji mkubwa.

Hatahivyo  amesema upatikanaji wa teknolojia hizo pamoja na majukwaa ya kuwaunganisha wadau unaweza kuongeza ushiriki wa vijana katika kilimo na kukifanya kuwa sekta yenye ushindani na fursa kubwa za biashara. SOMA: Wawekezaji wavutiwa sekta ya kilimo

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button