Vijana wafundwa, sasa kuja kivingine kwenye jamii
DAR ES SALAAM: Mkuu wa Itifaki na Uongozi wa Tanzania, Balozi Yusuph Mndolwa amesema mafunzo kwa Maofisa Itifaki vijana yanayotolewa na Taasisi ya Kweza International yanawajengea vijana uwezo wa kuwa na taswira nzuri.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo jijiji Dar es Salaam amesema ni lazima vijana waandaliwe katika misingi bora ili kuwa na mipangilio mizuri katika masuala wanayoshughulikia.
Kiongozi mshirika wa kweza international Bertha Mturi amesema ni muhimu kwa kila mtu kupata mafunzo hayo kwani husaidia kutengeneza taswira nzuri katika sehemu mbalimbali.
” Itifaki ni kwa kila mtu, itifaki ni kuanzia ngazi ya familia, kwahiyo haiishi kwa watumishi wa umma au taasisi flani hata mtu binafsi yeye mwenywe kutaka kujitambua”,amesema
Nae George Geofrey Mkurugenzi wa kampuni ya D& G events, Taasisi inayotoa huduma za itifaki, ametoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita kwa kufungua milango kwa vijana na kuwashika mikono pamoja na kuwapatia fursa.