Vijana watakiwa kuepuka mihemko na kulinda amani uchaguzi mkuu

ZANZIBAR : WAKATI Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar unatarajiwa kufanyika Jumatano, Oktoba 29, 2025, vijana wametakiwa kuepuka mihemko na badala yake kujikita katika kudumisha amani ya nchi kuelekea siku ya uchaguzi.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Zanzibar, Bwana Shaib Ibrahim Mohamed, katika kongamano la vijana lililoandaliwa na taasisi ya Pamoja Youth Initiative (PYI), lililofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort.
Amesema vijana ndio kundi kubwa linalolengwa kwa urahisi kupandikizwa chuki au kushawishiwa kuvuruga amani, hivyo ni jukumu lao kuwa mabalozi wa utulivu na umoja katika kipindi hiki nyeti. “Kumekuwa na tabia ya baadhi ya vijana kutumia mitandao ya kijamii si kutafuta fursa za maendeleo, bali kuchochea chuki hasa wakati wa uchaguzi. Machafuko mengi yameanza kama utani mitandaoni na kuishia kuleta madhara makubwa katika jamii,” alisema Shaib.
Amepongeza uongozi wa taasisi ya PYI kwa kuandaa majukwaa yanayowakutanisha vijana, viongozi wa dini na wanasiasa ili kujadili umuhimu wa amani na maelewano. “Tumeshuhudia nchi nyingi za Afrika zikikumbwa na vurugu zilizochochewa mitandaoni. Tunataka vijana wetu wajitambue na wajenge utamaduni wa kutumia mitandao kutafuta elimu, kazi, au miradi ya kujiajiri, si kusambaza maneno ya uchochezi,” alisisitiza.
Shaib pia amewahimiza vijana kujitokeza kupiga kura kwa amani na utulivu, wakitumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua viongozi wanaowaamini. SOMA: Wanaopiga kura Zanzibar leo watajwa
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa PYI, Rashid Mwinyi Rashid, amesema mazungumzo na vijana ni sehemu muhimu ya kuimarisha umoja, kuondoa mitazamo hasi na kujenga uelewa wa pamoja kuhusu nafasi ya vijana katika kulinda amani ya taifa. “Jukwaa hili ni sehemu ya juhudi za mradi wetu wa ‘Uchaguzi Bila Vurugu’, likiwa na lengo la kukuza ushiriki wa vijana na kuimarisha thamani za kidemokrasia,” alisema.
Washiriki 40 wakiwemo vijana, wazee, viongozi wa dini, na wawakilishi wa serikali za mitaa walihudhuria kongamano hilo, wakiahidi kuwa mabalozi wa amani kabla na baada ya uchaguzi.




I’m making over $25,000 a month working part-time. I kept hearing other people talk about how much money they were making online, so I decided to look into it. Well, it’s all true and has completely changed my life. This is what I do. Check it out by visiting the following link:
COPY THIS →→→→ http://Www.Work99.Site