Vijiji 17 havina umeme Tanzania

DAR ES SALAAM: JUMLA ya vijiji 12,301 kati ya vijiji 12,318 sawa na asilimia 99.86 pamoja vitongoji 32,827 kati ya 64,359 sawa na asilimia 51 vimeunganishwa na umeme nchini.

Hayo yameelezwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mha. Innocent Luoga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika ‘Mission 300’ kwenye Mkutano wa Wahariri na Wanahabari kuelekea mkutano huo jijini Dar es Salaam.

“Kupitia jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali, Tanzania imepata mafanikio mbalimbali kama
kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka MegaWatt (MW) 1,603.84 mwaka 2020 hadi kufikia MW 3,169.20 mwaka 2024,

“Kukamilisha mashine 6 kati ya 9 za mradi wa JNHPP ambao umefikia asilimia 99.55 Kukamilisha miradi ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi 1 MW185, Rusumo MW 80,

Kwa sasa, MW 1410 zinazalishwa kupitia JNHPP ukikamilika utazalisha MW 2115 za umeme unaozalishwa kwa mwaka kwa sasa MW 3169.

Mha. Luoga amesema hadi sasa jumla ya wateja milioni 5.2 tayari wameunganishiwa na umeme huku malengo ya nchi kwa mwaka ni kuwaunganishia wateja 500,000 kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitano (2025-2030) ambapo matarajio ni kuwafikia wateja milioni 7.7 kufikia 2030.

Lakini, kupitia Mkutano wa Mission 300 Watanzania milioni 13.5 watafikiwa na nishati ya umeme ambayo yaani karibu mara mbili ya malengo ya nchi ya miaka mitano.

Mission 300 inatarajiwa kusaini azimio la Mpango Mahsusi wa kitaifa ‘National Energy compact’ unaolenga kuwafikishia nishati ya uemem watu milioni 300 Afrika na kupitia wafadhili kama, Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) na wadau wengine wa maendeleo.

Habari Zifananazo

Back to top button