Vikundi 24,064 vyanufaika mafunzo usimamizi mikopo

DODOMA; SERIKALI imesema kipindi cha kuanzia Julai, 2024 hadi Januari 2026, jumla ya vikundi 24,064 vimepatiwa mafunzo ya usimamizi wa mikopo.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Reuben Kwagilwa ametoa kauli hiyo leo Februari 5, 2026 alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Daniel Mburarugaba, aliyehoji lini serikali imeweka utaratibu gani vikundi vinavyopata mikopo ya halmashaurikupatiwa mafunzo ya usimamizi, ili kuongeza ufanisi.

Serikali tayari imeweka utaratibu wa kutoa mafunzo ya biashara kwa wanufaika wa mikopo ya asilimia kumi kwa lengo la kuhakikisha mikopo hiyo inatumika kibiashara, kwa tija na kwa uendelevu.

Kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu za mwaka 2025 zinawataka wanavikundi kupata mafunzo ya ujasiriamali na mwongozo wa utoaji na usimamizi wa mikopo unaeleza kuwa vikundi vipate mafunzo ya siku sita ndani ya wiki sita kabla ya kupata mkopo na kuendelea kutoa mafunzo baada ya kupata mikopo.

“Lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuongeza maarifa, ujuzi na mitazamo chanya ya ujasiriamali ili waweze kuanzisha na kuendesha biashara endelevu, kuongeza kipato na kuboresha maisha yao.

“Aidha, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) imeandaa kitini cha wawezeshaji na wanufaika ili kurahisisha utoaji wa mafunzo hayo,” amesema Naibu Waziri.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com

  2. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button