Vinywaji, Urembo kuchangia Bima ya afya kwa wote

DODOMA – WAZIRI wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, Sura 147 ili kuelekeza asilimia 2 ya mapato ya ushuru wa bidhaa yanayokusanywa kutoka kwenye bidhaa za urembo, vinywaji laini na na vileo (bia na pombe kali) kwenye Bima ya Afya kwa wote.

Akisoma bajeti kuu ya serikali jijini Dodoma, Dk Mwigulu amesema lengo la hatua hiyo ni kuongeza fedha zitakazotumika kwa ajili ya kugharamia bima ya afya kwa watu wasio na uwezo na makundi maalum.

“Hii itaenda hususan wanawake wajawazito na watoto wa umri chini ya miaka mitano na hatua hii inatarajia kupeleka kiasi cha Sh milioni 18,800 katika Mfuko huo.

Habari Zifananazo

Back to top button