Viongozi wa dini nguzo ya amani uchaguzi mkuu

WATANZANIA wakiwa wamebakiza siku 16 kuanzia leo ili kuingia katika mchakato wa uchaguzi mkuu wa wagombea wa nafasi mbalimbali kuanzia urais, ubunge, uwakilishi na udiwani.
Tunaungana na wagombea hao pamoja na wadau mbalimbali kuwasisitiza Watanzania kuithamini amani iliyopo ili kuhakikisha uchaguzi unamalizika salama.
Katika kulifanikisha hilo wadau mbalimbali wana mchango mkubwa kuhakikisha amani hiyo inadumu wakiwemo viongozi wa dini.
Kutokana na umuhimu huo, ndiyo maana mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Hussein Mwinyi akizungumza katika hafla ya kuiombea nchi iliyotayarishwa na Ofisi ya Mufti Mkuu kwa kushirikiana na walimu wa madrasa na mashehe iliyofanyika Tunguu, Wilaya ya Kati Unguja alisema nchi inaingia katika kipindi kigumu cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, hivyo viongozi wa dini wanatakiwa kuiombea dua ili uchaguzi ufanyike kwa amani na utulivu.
Tunaungana na Dk Mwinyi kuendelea kuhimiza wanasiasa, viongozi wa dini pamoja na waandishi wa habari, makundi ambayo yana ushawishi mkubwa kuhubiri amani kipindi chote kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Ukweli ulio dhahiri ni kuwa katika jamii nyingi duniani, viongozi wa dini wamekuwa nguzo muhimu ya kuhakikisha maadili yanashamiri, mshikamano wa kijamii na kuhamasisha amani na ndivyo ilivyo pia kwa Tanzania na mataifa mengine ya Afrika.
Viongozi wa dini kwa nafasi yao wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi kwa njia zisizoegemea upande wowote, wakihubiri amani, mshikamano na uwajibikaji.
Tunawakumbusha Watanzania kuwa uchaguzi ni nguzo ya demokrasia lakini ni jambo lisilopingika kuwa kipindi cha uchaguzi huambatana na hisia kali, misuguano ya kisiasa na wakati mwingine machafuko.
Katika mazingira kama hayo, viongozi wa dini wana nafasi ya kipekee ya kuwa wapatanishi kwa sauti zao za busara na neema waliyopewa na Mungu.
Hivyo tunapenda kuwasihi watumie mimbari za ibada kuhubiri umuhimu wa kudumisha amani, kuepuka lugha za chuki na kuwahimiza waumini wao kushiriki uchaguzi kwa njia ya amani, uadilifu na utulivu.
Tunaamini viongozi wa dini wakiielimisha jamii hasa katika masuala ya haki za kidemokrasia, umuhimu wa kupiga kura na kuepuka propaganda potofu, uchaguzi utafanyika kwa amani na kukamilika bila misuguano ya aina yoyote.
Viongozi wa dini ni kundi linaloaminika na watu wengi, hivyo wakitumia nyumba za ibada kusisitiza amani kwa waumini wao ujumbe utapenya kwa haraka na kuleta mapokeo chanya kwa jamii.
Ni matumaini yetu pia kuwa viongozi wa dini watakuwa wapatanishi na kiunganishi baina ya vyama vya siasa, wananchi na vyombo vya dola ili kuleta mazingira yenye maelewano na maafikiano na kumaliza mchakato wa uchaguzi huku amani yetu ikiendelea kudumu.
Msisitizo wetu pia ni kuwaomba viongozi wa dini kutoegemea upande wowote ili kujenga uaminifu mbele ya waumini wao na kuepuka kuwa sehemu ya kuchochea mgawanyiko kwani ni wajibu wao kuwa taa ya maadili kwa jamii bila kuwa sehemu ya mpasuko wa kisiasa.
Tuanaendelea kusisitiza kuwa mchango wa viongozi wa dini katika mchakato wa uchaguzi na kulinda amani ni wa muhimu mno, hivyo ni wajibu wa jamii, serikali na vyombo vinavyosimamia uchaguzi kushirikiana nao ili kuhakikisha kuwa uchaguzi hauwi chanzo cha mgogoro bali msingi wa maendeleo na amani ya kudumu.
MAKAFEEL CITY UNDER CONSTRUCTION
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com
MAKAFEEL CITY UNDER CONSTRUCTION MAN AT WORK
MAKAFEEL CITY UNDER CONSTRUCTION MAN AT WORK USING FORCE PROJECT
MAKAFEEL CITY UNDER CONSTRUCTION MAN AT WORK USING BLACK LABEL
MAKAFEEL CITY UNDER CONSTRUCTION MAN AT WORK WITH $45,000,000,000 0N BOARD
MAKAFEEL CITY UNDER CONSTRUCTION MAN AT WORK USING WHITE LABEL