Viongozi wamuaga Lukuvi kwa heshima

VIONGOZI mbalimbali wa Serikali, siasa na wananchi wamejitokeza kumzika aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi, katika kijiji cha Idodi, mkoani Iringa.

Mazishi hayo yaliyofanyika Machi 31, 2026, yalihudhuriwa na Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, pamoja na viongozi wengine wa Serikali na CCM. Viongozi wengine ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira, wabunge na viongozi kutoka ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika ibada ya mazishi, Spika Mstaafu, Anna Makinda, alisema: “Marehemu Lukuvi atakumbukwa kwa utendaji wake wa vitendo na kujitolea kwake katika kuwahudumia wengine bila ubinafsi.” SOMA: BURIANI WILLIAM LUKUVI, HATIMAYE AZIKWA LEO KIJIJINI IDODI IRINGA

Naye Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, alisema:“Marehemu alikuwa kiongozi wa karibu na wananchi wake na mwenye unyenyekevu, akihudumu kwa ukaribu mkubwa na wananchi wa Jimbo la Isimani.”

Kwa upande wake, Wasira alisema:“Lukuvi alikuwa kiongozi mwenye uzalendo. Vijana wa CCM wajifunze historia yake ya uongozi iliyoanzia ngazi za chini hadi kufikia nafasi za juu.”Marehemu Lukuvi alifariki dunia Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa alipokuwa akipatiwa matibabu ya moyo.

 

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I get paid over $220 per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. the potential with this is endless…,

    This is what I do……. http://www.giftpay7.vip

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button