Vipaumbele 3 vyajadiliwa afya ushirikiano Uingereza na serikali

DAR ES SALAAM: WATAALAMU wa Afya kutoka Tanzania na Uingereza leo wamekutana jijini Dar es Salaam kujadili vipaumbele vitatu vya Mkataba wa ushirikiano baina ya pande zote ili kuboresha huduma za afya nchini.

Maeneo ya ushirikiano yaliyolengea ya vipaumbele ni utoaji huduma nchi ikiwemo huduma za tiba ,kufanya tafiti ili kugundua vitu vipya na kujengeana uwezo na kujifunza kutokana na utofauti wa mazingira na maendeleo ya matibabu.

Akizungumza wakati wa Kongamano la siku moja Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya, Dk Hamadi Nyembea amesema baada ya majadiliano hayo pia wataangalua eneo la uwekezaji kwenye viwanda vya uzalishaji dawa na vifaa tiba ili kuleta unafuu kwa Tanzania.

“Tutajikita zaidi kwenye maeneo ya tafiti,huduma za afya na mafunzo ,tunajadili mada mbalimbali pande zote na taasisi nyingi zimefika lengo ni wataalamu waweze kujadili na kubadilishana mawazo kuona jinsi sayansi ya matibabu inavyoenda.

Amesema kutokana na kongamano hilo wanategemea watajifunza kwa pamoja na taasisi za hapa na huko na kushirikiana katika matibabu.

“Jana walitembelea kwenye taasisi zetu wamefurahi na kuahidi kuendelea kushirikiana na sisi kwenye kwenye tiba ili kuwe na uwekezaji kwenye dawa na vifaa tiba,”amesisitiza.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili(MOI) Dk Lemeri Mchome amesema mashirikiano haya ni endelevu kwasababu katika afya kila siku mambo mapya yanatokea, huduma mpya zinatokea,tiba na vipimo vipya na teknolojia inakwenda mbele.

Dk Mchome amesema sasa kuna matumizi ya akili bandi katika matibabu na kutoa huduma za kiafya bila matibabu hayo hawawezi kwenda mbele.

“Katika kongamano hili tuna mambo ya kushiriki moja ni kujifunza wenzetu wamefanyaje kule na pili kuona sisi tulichofanya na kufikia kuona changamoto na baada ya hapo tutakaa meza moja kuona namna tunatatua hayo mapungufu chini ya wizara ya afya kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa wananchi.

Naye Prof Gideon Mlawa Kutoka Tanzania, UK healthcare Diaspora Association (TUHENDA) amesema wanakundi la wadau ambao wanajihusisha na mambo ya afya huko Uingereza ambapo maeneo waliyochagua ni elimu ya afya,tafiti na huduma za afya.

“Tulianza mwaka 2017 kama chama tukiwa tunaishi Uingereza na tumetembelea hospital mbalimbali kama Tumbi,Benjamin Mkapa,Mnazi Mmmoja na zingine na tumejifunza vingi kwa ziara zetu na tumeona hospital za huku zinafanya mambo mengi japo kuna uchache wa vifaa ukilinganisha na Uingereza.

Habari Zifananazo

Back to top button