Vitambulisho kidijitali kuwapa mikopo Machinga

KAMISHNA wa ustawi wa Jamii, Nandera Mhando amesema serikali imekuwa ikishughulikia kanzidata za Kitaifa ili kuwaunganisha wafanyabiashara ndogo ndogo wote na kuwatambua ili kurasimisha waweze kupata mikopo, rasilimali fedha na huduma za kijamii.
Akizungumza katika kongamano la Machinga la Hatua kwa Hatua na Mama, alisema kwa sasa serikali ipo katika mchakato mkubwa wa kuwa na vitambulisho vya kigitali ili kuwasaidia kupata mikopo yenye riba nafuu.
Alisema pia serikali imekuwa ikishughulikia kuunganisha wafanyabiashara ndogo ndogo wote, wakiwa Wamachinga, bodaboda, mama lishe ili kuweza kupata fulsa kupitia wilaya zao.
Nandera alisema serikali imekuwa ikiwapanga Wamachinga katika maeneo ya mijini ili kuwezesha upatikanaji wa fedha ili ziweze kuboresha miundombinu ya masoko katika halmashauri mbalimbali.
“Kongamano hili litumike kama jukwaa maalum la Serikali na taasisi za umma na binafsi zinazofanywa shughuli mbalimbali kwa ushirikiano na machinga ili kuweza kufafanua shughuli zilizopo maene hayo” alisema
Mkurugenzi wa Taasisi ya Hatua kwa Hatua na Mama, Amur Mussa alisema ameanzisha taasisi hiyo ili kuunga mkono jitahada za Rais Samia Suluhu Hassan kwa msaada ambao amekuwa akiwapa Wamachinga.
Alisema sasa hivi Wamachinga wanaweza kukopeshwa hadi milioni mbili bila ya kuwa nadhama, tena kwa kiwango kidogo cha riba hadi asilimia 9 .
Mkurugenzi wa Vijana Imara Antu Mfananga, alisema wameshirikiana na taasisi na taasisi ya Hatua kwa Hatua na Mama amesema lengo kuwakutanisha vijana, ili kufungua njia zao katika biashara.
“Tunaweza kuomba Serikali yetu kuwe na masoko ya usiku, kuna watu wengi na biashara nyingi ambazo zinawezankufanywa wakati watu wakitoka katika majukumu” alisema.
Mwisho



