SERIKALI imesema viti vyote 60,000 katika uwanja wa Mkapa vitaondolewa na kuwekwa vipya.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa ameeleza hatua hiyo ni mwendelezo mpango wa ukarabati wa uwanja huo ambao utakamila mwezi Agosti mwaka huu.
“Kama kutakuwa na ongezeko la muda tutawajulisha,”amesema Msigwa.
Akizungumza na Wasafi FM, Msigwa amesema baada ya kukamilika uwanja huo utatengenezewa utaratibu mpya wa kiuongozi.