VIVUTIO vya utalii vilivyopo Tanzania vimetajwa kuwa ni sababu ya kuandaa mkutano wa 53 wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC PF) mkoani Arusha, Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson ameeleza.
Akizungumza leo Julai 3, 2023 katika mkutano huo, Dk Tulia amefafanua kuwa mbali na vivutio vya utalii vilivyopo mkoani humo, hali ya hewa ni nzuri kwa wajumbe wengi wa mkutano huo.
Amesema kupitia mkusanyiko wa viongozi mbalimbali waliohudhuria mkutano huo, baadhi yao watapata fursa kwenda kwenye vivutio vya utalii vilivyopo Kilimanjaro, Arusha na Manyara ili kuutangaza zaidi utalii ikiwa ni mkakati wa Tanzania kutangaza utalii.
Mkutano huo unaofanyika kwa mara ya nne nchini, utadumu kwa siku saba, mada kadhaa zitajadiliwa ikiwa ni pamoja na njia za kisasa katika kilimo kama njia ya kuwa na uhakika wa chakula na ukosefu wa ajira kwa vijana.
Comments are closed.