Onyesheni nguvu ya mwanamke – Dk. Mongella

DAR-ES-SALAAM: WAKATI Dunia ikiendelea kuadhimisha miaka thelathini ya mkutano wa Beijing, Balozi Dk. Getrude Mongella amevunja ukimya na kuviomba vyombo vya habari kuandika habari zinazokuza nguvu ya mwanamke, badala ya kumwandika kama mnyonge.

“Vyombo vya habari vitoe picha za mwanamke shupavu, mwanamke mwenye uwezo wa kuchimba madini, mwanamke injinia, mwanamke wa kijijini ambaye anauwezo wa kutibu magonjwa,” alisema Dk. Mongella.

Aliongezea kuwa ,“ vyombo vya habari vinapaswa kutoa picha halisi ya nguvu ya mwanamke na visipofanya hivyo basi tutaendelea kudhalilika,” alisisitiza Dk. Mongella.

Akitoa tathmini yake kwa ufupi kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Beijing, Dk. Mongella amesema Tanzania imefanya vizuri katika maeneo mengi ya kumuwezesha mwanamke, ikiwa ni pamoja na masuala ya uongozi ambapo imepiga hatua kubwa, na sasa tuna Rais mwanamke.

“Ukija kuangalia katika masuala ya elimu, tumefanya vizuri. watoto wa kike sasa wanasoma mpaka elimu ya juu na mwamko ni mkubwa ukilinganisha na hapo awali,” alisema Balozi Dk. Mongella.

Aliongezea , “katika masuala ya uwezeshaji wanawake kiuchumi, wengi wamethubutu kujishughulisha na sio wale wa zamani waliokuwa wakisubiri kuletewa.” Alimalizia.

Miongoni mwa mambo yaliyokuwa yakipiganiwa katika mkutano wa Beijing ni kuona wanawake wengi wanakombolewa katika masuala mbalimbali kisiasa, kiuchumi, kimaendeleo, na kumuondoa katika dimbwi la udhalilishaji wa kijinsia.

SOMA: Rais Samia: Kinara wa usawa wa wanawake katika uongozi

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button