“Vyombo vya habari viweke wakalimani”

MAKAMU Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (Shivyawata) Tungi Mwanjala amesema Wizara ya Habari na Teknolojia ya habari iangalie uwezekano wa vyombo vya habari kuweka wakarimani wa lugha za alama.

Mwanjala amesema hayo leo jana kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Viziwi Duniani ambapo kitaifa yalifanyika mkoani Shinyanga.

“Vyombo vya habari vile vya kitaifa vikiweka wakarimani hata viziwi wataweza kupata habari kwa muda kufahamu maeneo yote tofauti na ilivyosasa,” amesema Mwanjala.

Advertisement

Mwajala amesema wanaiomba Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kuwepo na mitaala na usimamizi wa ufundishaji wa viziwi kwa kuanzia darasa la awali hadi vyuoni.

SOMA: Katambi atoa maelekezo ukaguzi mipakani

“Changamoto iliyopo viziwi kufundishwa kama watu wengine wenye kusikia na kuwafanya wafeli kwenye mitihani yao ya mwisho na muongozo ungewezeshwa ili wanafunzi wafuate”alisema Mwanjala.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi amesema serikali ina mipango madhubuti kuhakikisha inaondoa changamoto zinazo wakabili walemavu wote ikiwemo viziwi.

Serikali imeanza kufundishwa wataalamu wa lugha ya alama karibu makundi mengi muhimu nakutaka kuona maeneo ya taasisi za umma na dini yanakuwa na wakarimani.

/* */