Vyombo vya moto vyatakiwa kukaguliwa kuepuka ajali

WAMILIKI wa magari hasa ya abiria wamekumbushwa kujenga tabia ya kuvifanyia marekebisho ya mara kwa mara vyombo hivyo hasa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ili kuepusha ajali zinazoweka kuepukika.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Karimkee Group, Amit Singh wakati wa uzinduzi wa kituo kipya cha kisasa cha kutoa huduma za kisasa kilichopo Posta, Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo leo, Amit amesema kuwa msukumo mkubwa wa kufungua kituo hicho ni kuisadia serikali kuepukana na ajali za mara kwa mara hasa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

Advertisement

“Tunaiunga mkono serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Hassan katika kuepusha ajili za barabarani ndiomaana tumezindua kituo hiki cha huduma lengo ni kutaka kiviweka vyombo wanavyotumia wasafiri viko salama na huduma zetu zinamhakikishia msafiri kufika salama anakokwenda,” amesema Amit.

Kiongozi huyo amesema wamejipanga kutoa huduma bora na yakisasa lakini pia kwa garama nafuu ambayo itawawezesha wateja wao kufurahia huduma zao.

Aidha mkurugenzi huyo amesema kuzindua kituo hicho wameweza kuzalisha ajira mpya 32 katika vituo viwili walivyoanza navyo vya Posta na Mikocheni , Dar es Salaam.

Kampuni hiyo inajivunia kuwa na uzoefu wa miaka 200 katika kutoa huduma kwenye sekta ya usafirishaji na kuuza vipuri na vilainishi mbalimbali vya magari nchini Tanzania.