Vyombo vya ulinzi vyatakiwa kuibua vipaji shuleni

VYOMBO vya ulinzi na usalama vimetakiwa kuweka mpango mahususi wa kupata vijana wenye vipaji wakiwa shule za sekondari na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Akizungumza leo mkoani Mtwara wakati wa kufunga michezo ya majeshi mwaka 2023 iliyofanyika kitaifa mkoani hapa, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amesema ili kupata viwango vya wachezaji bora wa kuwakilisha Kimataifa na Kitaifa ni vyema vyombo hivyo vikatilia mkazo suala hilo.

Amesema juhudi za kuendesha michezo katika kambi kwenye sehemu zao za kazi ziendelee kuimarishwa na kuendelezwa ili kuweza kupata viwango hivo wachezaji waliyokuwa bora.

Advertisement

“Kwa kuwa askari wengi ni vijana na wenye nguvu wana uwezo mkubwa wa kuwakilisha Taifa katika michezo mashindano mengine ya Kimataifa maendeleo ya sekta yote inategemea jinsi ambavyo sekta ya michezo inavyoimarisha kiutawala na mafunzo mahili ya wanamichezo.” amesema Waziri Sagini.

Meja Jenerali Rajabu Mabele Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) amesema kazi ya Jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kuwaandaa Vijana wa Kitanzania ili waweze kuwa wazuri kwa kila kitu lakini pia waweze kitumika kwenye vikosi vingine vya Ulinzi na Usalama kama vile Magereza, Polisi na vingine.

“Kwahiyo Jeshi hili la Kujenga Taifa ni mtambo wa kuwaandaa Vijana, tunazalisha Vijana wenye vipaji kwa ajili ya kwenda kutumika kwenye Majeshi mengine”,amesema Mabele

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BAMMATA) Brigedia Jenerali Suleiman Gwaya amesema kubwa katika michezo hiyo ni kujenga ushirikiano kwani wameweza kuwa pamoja na kufurahi baina yao kutokana wengi wao wemeweza kutoka na ushindi kwenye mashindano hayo lakini pia kuja Mtwara kwao ni chachu kutokana wameweza kuwaonyesha Wanamtwara kwamba Askari hao siyo tu katika suala la bunduki pekee bali hata michezo.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas ameshukuru  michezo hiyo kufanyika mkoani humu kwani kumesaidia kuleta ukaribu kati ya Wananchi wa Mkoa huo na Majrshi hayo.

Michezo hiyo ilizinduliwa rasmi Februari 9 mwaka huu na kuhitimishwa leo hii Februari 21 2023 ambapo michezo 10 ilishindamishwa katika viwanja mbalimbali mkoani humo ikiwa ni pamoja Chuo cha Ualimu (TTC), Ufundi na Nangwanda kwa michezo ya riadha, mpira wa pete, judo na mingine.

/* */