Yvonne Chakachaka kutoa elimu ya hakimiliki kwa wasanii

DAR ES SALAAM: Meneja Mradi wa Taasisi ya Utamaduni na Maendeleo Afrika Mashariki (CDEA), Angela Kilusungu, amesema ujio wa mwanamuziki mkongwe kutoka Afrika, Yvonne Chakachaka, nchini Tanzania unalenga kutoa elimu na kuhamasisha wasanii kuhusu umuhimu wa kulinda na kunufaika na haki za kazi za muziki.
Kilusungu amesema hayo leo Dar es Salaam, wakati akimpokea Chakachaka, ambaye amewasili nchini kwa ajili ya kushiriki katika Jukwaa la Mashariki la Creative Economy Expo 2026, linalotarajiwa kuanza kesho na kuendelea hadi Agosti 21, 2026, Mlimani City.

Amesema Chakachaka, ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Watunzi wa Muziki Barani Afrika (SIZAC), amekuja kutoa ujumbe maalum kuhusu Copyright Friendly Label, hususan katika kuhakikisha wanamuziki wanapata haki zao pale kazi zao zinapotumika katika matamasha, michezo na matukio mbalimbali.
“Tumekuja kutoa elimu na kuipa moyo jamii ya wanamuziki wa Tanzania waweze kunufaika na michuano ya kimataifa ambayo tunaiandaa nchini,” amesema Kilusungu.
Ameeleza kuwa ujio huo ni muhimu zaidi kutokana na maandalizi ya Tanzania kwa michuano mikubwa ya kimataifa, ikiwemo mashindano ya soka yanayotarajiwa kufanyika nchini, ambapo matumizi ya kazi za muziki yatakuwa makubwa katika maeneo mbalimbali.
Kilusungu amesema kuchaguliwa kwa Chakachaka si kwa bahati, bali kutokana na nafasi yake katika SIZAC, taasisi inayolenga kuelimisha umma, serikali na watumiaji wa kazi za muziki kuhusu wajibu wa kutoa stahiki kwa wasanii na watunzi.
Amesema elimu hiyo itasaidia kuhakikisha taasisi, waandaaji wa matamasha na michezo pamoja na maeneo mbalimbali yanayotumia muziki yanafuata taratibu za kisheria na kuhakikisha mirabaha inawafikia wahusika.
Aidha Kilusungu ametoa rai kwa jamii ya burudani na wanamuziki nchini kujisajili katika taasisi zinazohusika na ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha, ili kupata uthibitisho wa matumizi ya kazi zao na kunufaika pale kazi hizo zinapotumika.
“Chochote ambacho wanakilipa kinaenda kutoa mirabaha kwa wanamuziki ambao wataweza kushiriki kwa namna moja au nyingine,” amesema.
Aidha, amewahimiza wadau wa muziki na ubunifu kufika katika Jukwaa la Mashariki la Creative Economy Expo 2026 ili kupata elimu na kufuatilia ujumbe utakaotolewa na Chakachaka kuhusu haki za wasanii na matumizi sahihi ya kazi za muziki.
Amesema Chakachaka atakuwa miongoni mwa wageni muhimu katika jukwaa hilo, akibeba ujumbe wa kuhamasisha sekta ya muziki barani Afrika kuhusu umuhimu wa kulinda hakimiliki na kuhakikisha wasanii wananufaika na kazi zao.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com