Vyuo vikuu vyashauriwa kuzingatia ubunifu, teknolojia

MOROGORO.: WIZARA ya Viwanda na Biashara imevishauri vyuo vikuu nchini kuhakikisha vinaandaa wanafunzi kuwa wabunifu kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia na mapinduzi ya viwanda ili waweze kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa mara wanapohitimu masomo yao.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Exaud Kigahe amesema hayo wakati akimuwakilisha Waziri wake Dk Selemani Jafo, kufungua siku ya Chuo Kikuu Mzumbe na kambi ya ujasiriamali iliyofanyika Kampasi Kuu Morogoro .

Kigahe amekipongeza Chuo Kikuu hicho kwa namna kinavyotekeleza kwa vitendo agenda ya Serikali ya kutaka vijana kupatiwa elimu na ujuzi utakaowawezesha kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa baada ya kumaliza masomo yao.

“Nimefurahishwa na tukio hili kwani inaonesha namna chuo kikuu hiki kinavyotekeleza kwa vitendo agenda ya serikali ya kutaka vijana kupatiwa elimu na ujuzi na kuwapa vijana fursa za ubunifu kwa vitendo utakaowawezesha kujiajiri,” amesema Kigahe.

“Tumeona hivi karibuni Mheshimiwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan, amezindua sera mpya ya elimu ambapo vijana hususani wanafunzi wa shule za sekondari wanapatiwa mafunzo ya amali, lakini pia hivi karibuni Waziri Mkuu alisisitiza umuhimu wa Watanzania kwenda kusoma Vyuo vya Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwa lengo la kupata ujuzi wa masuala mbalimbali,” amesema Kigahe.

Naibu Waziri amesema ni wakati sahihi kwa vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na serikali kupitia taasisi zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara, kwa kutumia bunifu na ujuzi walionao kujikwamua kiuchumi.

Amewataka wanafunzi kuitumia fursa kama hizo kwa kufanya bunifu zinazoendana na kukua kwa teknolojia zitakazowezesha kutatua changamoto mbalimbali kwenye jamii na kuiwezesha Tanzania ya viwanda inayojitegemea kwa maarifa na teknolojia.

“ Sisi Wizara tunakipongeza Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuwatengenezea mazingira wanafunzi wa chuo hiki yanayohamasisha ubunifu, kujifunza mbinu za ujasiriamali, uwekezaji na biashara wakati wakiendelea na masomo yao chuoni” amesema Kigahe.

Kwa upande wake, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho Taalama, tafiti na ushauri elekezi ,Profesa Hawa Tundui akizungumza kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Profesa William Mwegoha ,amesema kambi hiyo hufanyika kila mwaka ikiwa na lengo la kuwapa wanafunzi uzoefu wa vitendo na kuwaandaa kwa maisha ya kujitegemea baada ya masomo.

“Tunataka vijana wanapohitimu wawe na ujuzi wa kutatua changamoto katika jamii hususan katika sekta za kilimo, maji na matumizi ya teknolojia kama akili mnemba (AI),” amesema Profesa Tundui.

Profesa Tundui amesema kambi hiyo ilianza Mei 7 na kufikia tamati Mei 9,mwaka huu iliwakutanisha wanafunzi, wahitimu, wafanyakazi wa chuo, makampuni mbalimbali na wadau wa maendeleo .

Amesema zaidi ya mawazo 10 ya biashara yaliwasilishwa, huku washindi wa tatu bora wakipata zawadi za fedha kwa mshindi wa kwanza Sh milioni moja wa pili Sh 700,000 na wa tatu Sh 500,000.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I was BROKE and desperate… now I make $3,000+ weekly from my couch! Just 30 days ago, I was stuck in a dead-end job, living paycheck to paycheck. Then I found this secret method—and everything changed Anyone can do this in their free time. Spots are LIMITED! Don’t miss out!

    Join now➤➤ 𝐖­𝐰­𝐰­.­𝐄­𝐚­𝐫­𝐧­𝐀­𝐩­𝐩­𝟏­.𝐜­𝐨­𝐦

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button