Waandamanaji Congo wachoma moto jengo la ubalozi wa Kenya

CONGO: WAFANYAKAZI wawili katika ubalozi wa Kenya katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa, walilazimika kutoroka na kutafuta hifadhi baada ya waandamanaji kuvamia jengo hilo na kuchoma moto.
 
Umati wa watu wenye hasira, wakilalamikia shambulio la waasi dhidi ya Goma, pia walishambulia balozi za Rwanda, Uganda, Ufaransa na Ubelgiji.
 
Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya ilieleza kusikitishwa na mashambulizi hayo, ikiyaita kuwa hayafai. SOMA: EAC kujadili mgogoro wa DR Congo
 
Wizara hiyo ilisema shambulio dhidi ya ubalozi lilitokea mchana, huku maafisa wa usalama wa Congo wakishuhudia lakini “hawakuchukua hatua yoyote kuzuia hali hiyo”.
 
Tukio hili linadaiwa kuwa ukiukaji wa sheria za kimataifa, kwani serikali za nchi wenyeji zinawajibika kulinda balozi.
 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button