Waandishi watakiwa kupata taarifa sahihi Uchaguzi Mkuu 2025

ARUSHA : WAANDISHI wa habari wametakiwa kutumia kalamu vizuri katika kipindi cha uchaguzi ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa vyanzo vya uhakika na kujiepusha na taarifa za upendeleo, uchonganishi na uchochezi.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha, Salumu Kally kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi katika mkutano wa wadau wa sekta ya habari na utangazaji Kanda ya Kaskazini kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.

Mkutano huo uliwakutanisha wanahabari kutoka mikoa ya Kaskazini (Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga), makamanda wa polisi wa mikoa hiyo, wakaguzi waandamizi wa polisi kata wa mikoa hiyo, maofisa habari na maofisa wa Idara ya Habari-MAELEZO kutoka Dodoma.

Akizungumza katika mkutano huo, Kally alisema iwapo wanahabari watajikita katika weledi wa taaluma yao katika kipindi cha uchaguzi ana uhakika uchaguzi utakuwa wa amani; wagombea watakaoshinda watashinda, wataoshindwa watakubaliana na matokeo.

Alisema wanahabari wanapaswa kuwa walinzi wa kweli katika kipindi cha uchaguzi na kutoa taarifa za kweli kutoka katika vyanzo vya uhakika vinavyotambulika kisheria na kimamlaka zenye lengo la kulinda amani na kutumia vyema kalamu kutekeleza maadili ya kazi yao katika kipindi chote cha uchaguzi.

Aliviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kushirikiana na waandishi wa habari kipindi chote cha uchaguzi kwa lengo la kulinda amani katika kipindi chote cha uchaguzi kwani ushirikiano ndio unajenga amani muda wote. Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya HabariMAELEZO, Rodney Thadeus aliwasisitiza wanahabari kuhakikisha wanapata taarifa za msingi na sahihi kwa watu sahihi katika kipindi chote cha uchaguzi kwani hilo ni muhimu katika muda wote wa uchaguzi.

Alisema katika kipindi chote cha uchaguzi kuanzia kampeni na siku ya utoaji matokeo waandishi wanaopaswa kutoa taarifa hizo ni wale waliosajiliwa na Bodi ya Ithibati (JAB) na kuonya wale watakaofanya kazi bila kusajiliwa kuwa wanakiuka sheria hivyo hatua zitachukuliwa dhidi yako. SOMA: “Waandishi ifuateni Tume Huru ya Uchaguzi”

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button