OFISA Madini Mkazi Mkoa wa Mtwara, Mhandisi Ephraim Mushi ametoa rai kwa wachimbaji wa madini mkoani humo kushiriki kikamilifu huduma za Jamii wakati wanapotekeleza majukumu hayo kwenye maeneo yao ya uchimbaji ikiwemo ujenzi wa shule na megine.
Akizungumza mkoani Mtwara Ofisa Madini Mkazi huyo amesema sheria ya madini inamtaka kila mchimbaji kushiriki ipasavyo kwenye utoaji wa huduma mbalimbali za Kijamii kwenye eneo linalofanyika huduma hiyo.
Hata hivyo wazingatie suala la ulipaji wa mrabaha kwa wakati na kufata sheria, Kaninu za uchimbaji wa madini kwani inasaidia kuepuka madeni na usumbufu usiyokuwa wa lazima siku za baadaye.
Amesema wachimbaji hao anapotekeleza shughuli zao hizo wanatakiwa watekeleze chini ya Sheria hiyo lakini pia masuala ya usalama na utunzaji wa mazingira katika maeneo hayo ya uchimbaji kwani usalama ni muhimu katika mazingira ya uchimbaji.
‘’Kukitokea tatizo lolote kwenye mgodi, mgodi unasimamishwa na ukisimamishwa kwa maana hiyo hakuna uzalishaji mwenye mgodi hapati chochote na Serikali hatuwezi kukusanya mapato sasa ili pande zote mbili zisipoteze mapato tuzingatie Sheria’’,amesema Mushi Khalfan Nassoro ni uchimbaji wa chumvi kwenye Halmshauri ya Wilaya ya Mtwara amesema agizo hilo lililotolewa na Serikali litazingatiwa ikiwemo ulipaji wa mrabaha kwa wakati ili wasipoteze mapato kwa pande hizo zote mbili.