Wadau wa ardhi wapewa somo

KUWEPO kwa ushindani wa mahitaji ya ardhi, migogoro itaendelea kuwepo, hivyo ni vema wananchi, wadau wa uhifadhi na serikali kuandaa mikakati ya namna ya kutatua migogoro hiyo, imeelezwa.

Akizunguza wakati wa kufunga warasha na Mkutano Mkuu wa 22 wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), mlezi wa Mtandao huo, Charles Meshack alisema wakati idadi ya watu inaongezeka huku ardhi ikiwa haiongezeki, ushindani wa kupata maji, ardhi ya kufugia, kilimo na mazao ya misitu kwa ajili ya mbao, kuni na mkaa utaendelea kuwepo.

Lakini akasema ni lazima mikakati iendelee kuwekwa ili kuhakikisha misitu inazidi kulindwa na hivyo kufanya matumizi endelevu ya misitu kwa sababu jamii ndio inayohitaji misitu na siyo kwamba misitu inawahitaji watu.

“Misitu tunaihitaji lakini lazima tuivune kwa njia endelevu na hivyo tujue tunapomaliza misitu hata kama ni kwa kufungua mashamba, basi tujue mabadiliko ya tabianchi yayatuadhibu,” alisema.

Meshack ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) aliwataka wawikilishi wa Mjumita kutoka Kanda mbalimbali nchini kuzuia pale wanapoona uharibifu wa mazingira unafanyika mbele yao.

“Sisi ndio tunakaa karibu na msitu. Tunawajua na kuwaona maharamia wa misitu.

buy bactrim online innomed.net/Images/SurgShots/jpg/bactrim.html no prescription pharmacy

Sisi ndio tunaona watu wanaharibu misitu hata kama viongozi wanapewa rushwa lazima tukatae.

buy clomiphene online innomed.net/Images/SurgShots/jpg/clomiphene.html no prescription pharmacy

Tusiishie kulalamika bali tuhakikishe misitu yetu inavunwa kwa utaratuibu na wanaokiuka tuwakamate,” alisema.

Mkurugenzi wa Mjumita, Rehima Njaidi alitaja malengo ya mkutano huo Mkuu uliofunguliwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja kluwa ni kujadili mafanikio na changamoto zinazowakumba wahifadhi wa misitu na kuja na maazimio ya pamoja kuhusu mikakati ya kuchukua.

Mjumita ina wanachama takribani 15,000 wanaoishi kandokando ya misitu ya asili, katika mikoa 13, wilaya 30 na malengo ya shirika hilo lisilo la kiserikali ni kufanya uhifadhi endelevu wa misitu ya asili.

buy neurontin online innomed.net/Images/SurgShots/jpg/neurontin.html no prescription pharmacy

Kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘Tushirikishe wanawake na vijana ili kuboresha uhifadhi wa misitu na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi’.

Habari Zifananazo

Back to top button