Wadau wafurahishwa onesho la utalii

WADAU mbalimbali nchini wamefurahishwa na onesho la Swahili International Tourism Expo (S!TE 2024 ) lililoandaliwa na Bodi ya Utalii kwa lengo la kuwaleta pamoja wadau wa utalii kujionea na kufanya manunuzi ya bidhaa za utalii.

Hoteli ya Kisiwa on the Beach iliyopo Zanzibar ni wadau waliofurahishwa na onesho hilo lililofikia tamati leo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Julius Kamau ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali kuwapatia watalii huduma bora za malazi ili kukuza uchumi wa nchi.

Advertisement

“Tutaendelea kushirikiana na Serikali ilikuwapatia malazi yaliyobora na kuongeza uchumi wa nchi kupitia fedha za kigeni.

Amesema kampuni imepata mafanikio mbalimbali ikiwemo kupata tuzo na kushika nafasi ya sita kwa Afrika. Aliongeza kuwa anaamini onesho lijalo litakuwa bora zaidi na kupata wanunuzi wengi zaidi .