Wadau wakutana kujadili biashara, uchumi Kigoma

KIGOMA; Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro amesema mkoa huo utatumia nafasi yake ya kuwa mkoa wa kimkakati kama lango la biashara ya kikanda nchi za maziwa makuu kutekeleza dhamira ya serikali ya kujenga uchumi imara na wenye ushindani unaochochewa na uwekezaji wa sekta binafsi.
Balozi Sirro amesema hayo katika mkutano na viongozi wa serikali, wawakilishi wa sekta binafsi, taasisi za fedha, vyama vya wafanyabiashara pamoja na washirika wa maendeleo waliokutana kujadili uwekezaji, biashara na ukuaji jumuishi wa uchumi kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika kufungua fursa za kiuchumi na kuhamasisha maendeleo jumuishi ya kiuchumi mkoani humo.
Amesema kutokana na mkoa huo kuwa jirani nan chi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Burundi, Zambia na Rwanda hali inayofungua fursa kubwa za uwekezaji, biashara na maendeleo ya viwanda ni dhamira ya serikali kuwekeza katika miundombinu muhimu, ili kuharakisha ukuaji wa uchumi wa mkoa huo.

Ametaja mambo hayo ni uboreshaji wa barabara, uimarishaji wa Bandari ya Kigoma, ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) sambamba na barabara kutoka maeneo ya uzalishaji kwenye kilimo vijijini.
Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Serikali ya Ubelgiji (ENABEL), Koen Goekint alisema kuwa mageuzi ya kiuchumi yaliyo jumuishi na endelevu yanahitaji ushirikiano mpana yakihitaji sekta binafsi kufungua milango na kuunda fursa sambamba na Serikali kuweka mazingira wezeshi ya biashara.

Amsema mazingira hayo yanahitaji taasisi za mafunzo kuandaa vijana kwa ajira na biashara za kesho, huku taasisi za fedha zikitoa huduma za kifedha kwa wale, ambao bado wana changamoto kufikia fursa za mikopo na uwezeshaji na kwamba washirika wa maendeleo wanapaswa kuunganishwa kama wawezeshaji, kuunganisha na kuchochea ushirikiano.
–




Interesting read! For live football scores, https://jogosdehoje.eu.com/ is the best resource I’ve found — real-time updates and stats. Highly recommend!