Wadau washauri wa bima kukutana Arusha

DAR ES SALAAM :Wadau mbalimbali wa bima kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajia kukutana katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa nane wa Chama Cha Washauri wa Bima Tanzania ( TIBA) kujadili masuala mbalimbali ya bima ikiwemo sheria mbalimbali za bima nchini.

Hayo yamesemwa na Rais wa chama hicho (TIBA), Okoth Oloo, leo jijini Dar es Salaam wakati alipozungumza na waandishi wa habari akisema kuwa mkutano huo utawakatunisha wadau mbalimbali wa bima nchini na kutoka Kanda ya Mashariki, Kusini na Afrika Magharibi .

Oloo amesema kuwa Kamishna wa Mamlaka ya Bima nchini Dk Baghayo Saqware anatarijiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo ambao pia wananchi pia wanaweza kushiriki .

Advertisement

“ Tumemuita Kamishina Mkuu wa Bima kwas ababu ndiye anayesimamia masuala ya sheria ya bima, ili tuweze kujadili sheria za bima nchini na kuchochea ukuaji wa biashara yake,” amesema Oloo

Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Julai 25-26  mwaka huu jijini Arusha umebeba Dhima ya : “Sheria ni Kichocheo cha Maendeleo na Ukuaji”, yenye lengo la kujadili namna sheria hizo zinavyoweza kuchochea ukuaji wa sekta hiyo nchini.

Kwa upande mwingine Oloo amesema mkutano huo pia utajadili mambo mbalimbali, ikiwemo uimara wa soko la sekta ya bima nchini, masuala ya udhibiti na usimamiaji wa sekta hiyo pamoja na kujifunza namna ya uendeshaji wa bima kutoka nchi zingine zitakazoshiriki.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa maandalizi wa Mkutano huo, Anna Lema amesema tayari maandalizi ya mkutano huo yamekamilika, na kuwataka wadau wa sekta ya bima na wananchi kwa ujumla kushiriki katika mkutano huo kwa kujisajili kupitia tovuti ya TIBA.

Naye Katibu Mkuu wa TIBA, Aliasaher Somji amesema wadhamini wa mkutano huo ni nyenzo muhimu inayosaidia kufikisha ujumbe kwa jamii kwa kutoa elimu ya bima kwa wananchi kukata bima kwaajili ya kulinda biashara na amaisha yao.