Wafanyabiashara: Sheria za kodi zifikirie wazawa

WADAU wa kodi wametoa mapendekezo kadhaa yakiwemo kuboresha mifu[1]mo na sheria ili kuboresha mazingira ya biashara. Wameshauri sheria za kodi zilenge kuleta unafuu kwa wafanyabiashara wazawa kuliko wageni katika ulipaji kodi ili kuongeza tija kwenye ukusanyaji wa mapato nchini.
Walisema hayo katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam jana kwenye mkutano wa kupokea maoni ulioitishwa na Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi. Walishauri kuwe na usimamizi kwenye sheria ya kodi kwa kampuni zinayojibadilisha ili kuzuia zisikwepe kodi na kuisababishia hasara serikali.
Pia, walipendekeza marekebisho katika mfumo wa kodi ya uthamini wa bidhaa wakidai kuwa umekuwa mwiba kwa wafanyabiashara. Wamependekeza kuwepo na mfumo wa kodi elekezi utakaoonesha gharama halisi ya malipo kutokana na mizigo inayoingia sokoni ili kulinda biashara za ndani.
Wafanyabiashara Kariakoo Katibu Mteule wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Renatus Mlelwa alisema wafanyabiashara wa Kariakoo wanateswa na ushuru wa forodha kutokana na mfumo wa uthamini wa mizigo inayoingia Kariakoo kutoka bandarini. Mlelwa alisema jedwali la kukokotoa ili kupata thamani halisi ya mzigo katika kila kipengele inafikia hadi 72.
“Huyu mfanyabiashara wa Kariakoo ili aweze kuwa na kontena la milioni 400 lazima awe na milioni 80 ambazo si sahihi kwa ajili ya kodi ya kuthamini mzigo wake na ikiwa atasema mzigo wake ni wa milioni 80 kodi ya forodha itakuwa milioni 32 hali inayoleta maumivu makubwa kwa wafanyabiashara,” alisema.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Soko la Kariakoo, Mfaume Mfaume amependekeza serikali ifanye mageuzi ya ndani ya kisera na kisheria ili kuwavutia wafanyabiashara kutoka mataifa ya Afrika Mashariki ili kuleta fedha nyingi za kigeni.
Wafanyabiashara wadogo (Wamachinga) Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wamachinga Tanzania, Stephen Lusinde alisema changamoto kubwa kwa wamachinga nchini ni uhaba wa maeneo ya kufanyia biashara ambayo kimsingi imekuwa iki[1]leta usumbufu na kusababisha wengi wao kupanga bidhaa katika mitaa. Lusinde ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamachinga Kariakoo alisema changamoto hiyo imekuwa ikiendelea licha ya jitihada zilizofanywa na serikali kuhakikisha wamach[1]inga wanapata maeneo kwa ajili ya kufanya biashara.
“Tumepisha maeneo mengi kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ambapo tulikuwa tunaambiwa tutatafutiwa eneo mbadala hadi leo hatujui hatma yetu kwani tumekuwa tunahangaika tuu pasi na ku[1]pata majibu stahiki,” alisema. Lusinde alisema kwenye eneo la DDC Kariakoo walielezwa waandae mchoro kwa ajili ya vizimba vya wam[1]achinga zaidi ya 6,000 lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.
Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) Katibu Mtendaji wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA), Raymond Samson alitoa ombi la kupunguzwa kwa malipo ya kuingiza basi jipya nchini kutoka asilimia 25 ya sasa hadi asilimia kati ya tano hadi 10.
Samson alisema wanaomba hivyo kwa kuwa mfanyabiashara analipa malipo mengi kabla ya basi kufanya kazi. Aidha, alipendekeza kuwe na kodi mfuto na kwa mwaka alipendekeza kulipa Sh milioni moja kwa kila basi. Kwa upande wa malipo kwenye stendi za mabasi alishauri pawepo na dirisha moja la malipo chini ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili mmiliki akadiriwe kodi na anapokata leseni ya biashara tozo hiyo ijumlishwe kwenye leseni. “Hii itapunguza usumbufu wa mabasi kuingia na kulipa tozo kila kituo kwani imekuwa ikipoteza muda mwingi na usumbufu mkubwa kwa abiria kwani basi litalazimika kuingia kila kituo hata kama hakuna mtu anayeshuka,” alisema Samson.
Chama cha Mabaharia Dar es Salaam Katibu wa Chama cha Mabaharia, Mkoa wa Dar es Sa[1]laam, Frank Linkamba alisema mfumo wa sasa hauwaruhusu mabaharia kulipa kodi hivyo serikali imekuwa ikipoteza mapato. Linkamba alisema maba[1]haria wengi takribani asilimia 80, wanafanya kazi nje ya nchi na hawalipi kodi yoyote kwa sababu mifumo ya ulipaji kodi haiwatambui.
“Baadhi ya nchi za wenzetu wanakuwa na madawati ya ufatiliaji ambapo baharia ataonesha mkataba wake wa kazi na mshahara ili akatwe kodi. Hii itaongeza ukusanyaji wa kodi,” alisema. Linkamba alisema ikiwa serikali inamkata mwalimu kodi katika mshahara wa Sh 600,000 kwa nini baharia anapata dola za Marekani 2,500 anaachiwa? “Kwa sababu kima cha chini cha baharia analipwa dola 400 na hizo ni ngazi za Kitanzania tu, ukienda huko analipwa dola 1,500 hadi 2,000 na huyo ni baharia wa darasa la saba au kidato cha nne,” alisema.
Linkamba alisema kwa upande wa Zanzibar, mabaharia wote wamewekewa mfumo wa kuchukulia mishahara yao kwenye Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) hivyo serikali inapata fedha za kigeni lakini Tanzania Bara serikali haipati chochote. “Sisi tunaishauri serikali ili Watanzania waweze kulipa kodi, irekebishe mfumo wa ulipaji kodi uwe mzuri kwa sababu mfumo ukiwa mzuri mabaharia watalipa kodi kwa hiyari na taifa litapata fedha za kigeni,” alisema.
Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Mwakilishi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, Fredirick Lutindi anayefanya shughuli zake katika Soko la Kariakoo mkoani Dar es Salaam alisema tatizo linalo[1]sumbua wafanyabiashara wanaopitisha mizigo yao bandarini ni kutosomana kwa mifumo inayohusika. Lutindi alisema kwa kuwa kodi zinawekwa katika viwango viwili kwa maana ya cha juu na cha chini imejenga mazingira ya mazungumzo kwa watendaji ambao si waadilifu.
“Naiomba serikali kodi zetu zote zisiwe na kiwango cha chini na cha juu badala yake kuwe na kiwango kimoja ili kuondoa mfumo wa mazungumzo yanayoleta mazingira ya rushwa,” alisema Lutindi. Alisema changamoto nyingine ambayo inawakwaza wafanyabiashara ni kodi ya huduma ambayo badala ya kulipa kodi moja kwa huduma zote kila huduma inalipiwa kodi yake na kusababisha mfanyabiashara kuwa na alipe kodi nyingi kwa kitu kimoja.
Pia, alisema kiwango cha kodi hiyo kinachotozwa si rafiki kwa sababu inaanzia 0.1 hadi 0.3 hali inayokaribisha mazungumzo ya kupeana rushwa kwa mtu ambaye si mwadilifu. “Mimi naomba seri[1]kali iangalie namna ya kuifuta kabisa kwa sababu inawaumiza wafanyabiashara lakini pili inatoza kwenye mauzo ghafi hivyo inaathiri mtaji wa mtu. Pia, kama ni lazima hiyo kodi iwepo, iingizwe kwenye kodi ya leseni au iwe kodi ya kiwango kimoja,” alisema Lutindi.
Alisema changamoto nyingine kwa wafanyabiashara ni kamatakamata inayofanywa na kikosikazi katika maeneo ya Kariakoo. Lutindi alidai kuwa taifa zima linategemea Kariakoo na kunapokosekana utulivu Kariakoo pia nchi nzima inakosa utulivu. Alisema kwa kuwa nchi nane zinazoizunguka Tanza[1]nia zinategemea Bandari ya Dar es Salaam ikiwa Kariakoo itakosa utulivu hata nchi hizo pia zitakosa utulivu.
Lutindi alisema tatizo lingine ni matumizi ya nguvu katika kukusanya kodi akidai kuwa yanaikosesha serikali mapato kwa sababu watu watafunga bishara kuhofia kupoteza mali zao.
Kwa mujibu wa Lutindi, ikiwa matumizi ya mabavu yataachwa ni wazi kuwa watu wengi watakipa kodi kwa hiyari yao hali itakayosababisha serikali kupata fedha nyingi zaidi na pia kuingiza fedha nyingi za kigeni. “Jambo lingine ni utitiri wa kodi, kodi ni nyingi mno, natamani kodi hizi ziwekwe pamoja ili zikusanywe na watu wachache kuliko ilivyo hivi sasa ambapo wanaokuja kukusanya kodi ni wengi ku[1]liko idadi ya wafanyabiashara wenyewe. Tungependa wateja wawe wengi kuliko waku[1]sanya kodi,” alisema.
Aliiomba serikali itengeneze sera na mazingira rafiki kwa ajili ya wafanyabiashara wa ndani ili kuzuia wageni kuja kupora ajira za wazawa ili wageni waje kufanya kazi ambazo Watanzania hawaziwezi lakini kazi ndogondogo zifanywe na Watanzania. Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Dar es Salaam, Peter Mareale alishauri serikali irekebishe mfumo unaotu[1]miwa kwenye kukusanya kodi wa ankara kwani unaleta mchanganyiko hasa kwenye malipo.
Mareale alisema kwa sasa hakuna sheria mama ambayo inaelekeza muda halisi wa kuwasilisha zile fedha ambazo mtu amefanya huduma. Alihoji ni kwa nini serikali idai ndani ya siku 20 wakati hakuna mfumo unaolinda au unaoeleza malipo kwa siku hizo 20. Alisema changamoto hutokea wakati mfanyabiashara anapokuwa amelipa ile Kodi ya Ongezeko la Thamani serikali akitegemea kulipa ankara



