Wafanyakazi kampuni ya kufua vyuma wapata faraja

HATIMAYE wafanyakazi wa kampuni ya kufua vyuma na kutengeneza matanki ya maji ya Lodhia Group ya Jijini Arusha waliogoma wakidai masahi yao kilio chao kimesikilizwa baada ya uongozi wa kampuni hiyo kuongeza mshahara na nyongeza za malipo ya saa za ziada.

Awali wafanyakazi zaidi ya 700 wa Kampuni hiyo waligoma kufanya kazi kwa siku mbili kwa madai ya mshahara wa shilingi 150,000 hautoshi ,vitendea kazi hakuna,kudhalilishwa kwa matusi ya nguoni na uongozi wa juu hatua iliyofanya Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtehengerwa kwenda katika kiwanda hicho kusikiliza kero za wafanyakazi hao.

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara kati ya wafanyakazi,uongozi wa Lodhia Group chini ya mwenyekiti wa Aruni Lodhia, wakuu wa idara ya kazi na Osha,Lodhia aliahidi kupandisha mshahara hadi shilingi 180,000 na huduma zote za afya kwa mfanyakazi zitaboreshwa na nyongeza za masaa ya ziada zitalipwa kwa wakati.

Advertisement

Mwenyekiti Lodhia aliwataka wafanyakazi kurudi kazini kesho kuendelea na kazi na kuahidi kukutana mara mbili kwa mwaka kuzungumza changamoto za kiwanda kati ya wafanyakazi na menejimenti lengo kutaka kufanya kazi kwa ushirikiano bila kumwonea mtu kwani sote ni watanzania.

‘’ Ninaongeza mshahara kutoka shilingi 150,000 hadi shilingi 180,000 nitalipa masaa ya ziada nitaboresha huduma ya afya ikiwemo kupewa maziwa mara mbili kwa wiki na huduma zingine za maeneo ya kazi yataboreshwa kwa masilahi ya wafanyakazi’’ alisema Lodhia

Wale wote waliochukuliwa hatua kwa kukosa kwenda kazini na kukatwa mshahara warudishiwe pesa zao na kila kitu kiende sawa kwa kushirikiana lengo kila mmoja apate masilahi.

Mkuu wa wilaya Arusha, Felician Mtehengerwa aliwataka wafanyakazi kesho kuendelea na kazi na wale viongozi wa Lodhia Group wenye kutishia wafanyakazi na kauli chafu watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria kwani hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Mtehengerwa alisisitiza kwa kampuni ya Lodhia Group kulinda masilahi ya wafanyakazi kwa kulipa kile wanachostahili na wakati muafaka ili kila mfanyakazi aweze kufanya kazi kwa uhuru na amani akiwa kazini na unyanyasaji na udhalilishwaji hataki kuusikiliza.

‘’Hapa nataka kazi ifanyike kwa wafanyakazi kujituma na menejimenti kulinda masilahi ya wafanyakazi na hataki kusikia udhalilishwaji ,unyanyasaji na kutishiana kwani hakuna mtu aliye juu ya sheria’’alisema Mkuu wa wilaya

Mmoja wafanyakazi wa Lodhia Group aliyejitambulisha kwa jina la Martin Antony alisema menejimenti ya kampuni hiyo haiwajali wafanyakazi na kuwaacha bila kuwajali ikiwa ni pamoja na kutolipwa mshahara kwa wakati ,vitendea kazi hakuna,masaa ya ziada hayalipwi hivyo kuwa katika maisha magumu na familia zao.

Mfanyakazi mwingine Juma Rajabu yeye alisema wafanyakazi wenye asili ya kihindi wamekuwa na tabia za kuwadhalilisha na kuwatukana wafanyakazi wa kiafrika hatua ambayo haiwapendezi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *