Wafuasi wa CHADEMA waliokamatwa wafikia 500+
Deprecated: htmlspecialchars(): Passing null to parameter #1 ($string) of type string is deprecated in /home/habarileoacc/public_html/wp-includes/formatting.php on line 4732
DODOMA – Idadi ya Wafuasi na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokamatwa na Jeshi la Polisi kufuatia katazo la kongamano la vijana katika uwanja wa Ruanda Nzovwe jijini Mbeya imefikia 520.
Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Awadh Haji imesema waliokamatwa ni pamoja na Tundu Lissu, John Mnyika, Joseph Mbilinyi, Twaha Mwaipaya na Moza Ally.
SOMA: CCM yaitaka CHADEMA kuacha undumilakuwili
Wengine ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, na Kiongozi wa Baraza la Vijana Chadema, John Pambalu.
Wafuasi 375 wa Chadema na viongozi walikamatwa Agosti 11 na Wengine 145 walikamatwa Agosti 12, taarifa ya Polisi imesema. Waliokamatwa wengi wao walikuwa katika mikoa ya Morogoro (28), Iringa (109), Njombe (60), Dar es Salaam (19), Pwani (41), Rukwa (30) na Songwe (51).
Tayari Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka serikali kuwaachia huru viongozi na wafuasi hao ili kuruhusu maridhiano ya pande zote.
Katibu Mkuu cha CCM, Balozi Emmanuel Nchimbi alisema akiwa Mjini Geita jana kuwa viongozi hao na wanachama wa Chadema wanapaswa kuachiwa ili CCM na Chadema ziweze kuzungumza juu ya changamoto hiyo.
CP Haji amesema mbali na kukamatwa kwa wajumbe hao, Polisi pia ilikamata magari 25 katika mikoa mbalimbali 20 yakiwa ni aina ya Toyota Coaster.
Deprecated: htmlspecialchars(): Passing null to parameter #1 ($string) of type string is deprecated in /home/habarileoacc/public_html/wp-includes/formatting.php on line 4732