Wafugaji Longido watakiwa kupuuza fitna

ARUSHA: CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimewataka wafugaji wa waliopo Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha kujitenga na fitna zinazojengwa na kusambazwa na wanasiasa.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla ametoa kauli hiyi Septemba 5 jioni alipozungumza na wananchi wa jamii hiyo akiwa katika kata ya Mundarara iliyopo wilayani Longido akiwa ziarani mkoani Arusha.

Advertisement

Makalla ameeleza na kuwatoa hofu wafugaji kwamba serikali haina mpango wa kuwaondoa kwenye maeneo yao na kuwasisitiza wananchi hao wajitenge na fitna zinazosambazwa na wanasiasa ambao hawaishi katika eneo hilo.

SOMA: Benki yazindua akaunti ya mfugaji

“Fitna hizi naomba mzipuuze, naomba muwe na imani na Rais Dk Samia Suluhu Hassan, naomba muwe na imani na serikali ya CCM, kwa sababu fitna hizi zinasambazwa na watu ambao sio wafugaji, fitna hizi zinasambazwa na watu ambao makazi yao ni nje ya Longido wanaishi mjini na sio hapa, endeleeni kuamini kauli ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan”