Wageni watajwa ongezeko la VVU Manispaa Moro,  Ifakara

MOROGORO; Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Dk Mussa Ali Mussa amesema ongezeko la maambukizi mapya ya VVU Manispaa ya Morogoro na halmashauri ya Mji Ifakara  kunatokana na kuwepo kwa  wageni wengi.

Dk Mussa amesema hayo mbele ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya  Bunge ya Afya  na Masuala ya Ukimwi,  Dk  Zeyana Abdallah Hamid,  ilipofanya ziara mkoani Morogoro  na kutembelea   Kituo cha Afya Kingolwira , Manispaa ya Morogoro  pamoja na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) .

Amesema  kuongezeka kwa maambukizi mpaya kwa Manispaa ya  Morogoro kunachangiwa na ujio wa  wageni wengi  pamoja uwepo wa  vyuo vingi  vyenye  kukusanya vijana wengi,  jambo ambalo linaweza kuchangia ongezeko la  mambukizi mapya ya VVU.

Kwa upande wa Mji Ifakara Dk Mussa ameeleza wenyewe ni  m ji wa kibiashara ambaao pia unajumisha makabila mengi na  wengi wao wanavutiwa  na shughuli za  kilimo , biashara pamoja na  kuwepo wafugaji wenye wenye kuhamahama.

Dk Mussa amesema kwa sasa juhudi zinaendelea kuchukuliwa, zikiwa na utoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali  ya kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi mapya.

Naye Mratibu wa Ukimwi na Magonjwa ya Ngono na Homa ya Ini Mkoa wa Morogoro , Dk Shigela Marco, amesema  utafiti wa Tanzania HIV impact Survey (THIS) wa Mwaka 2022/2023 ulionesha maambukizi ya VVU kwa mkoa huo ni  asilimia 3.3 , wanawake asilimia 3.6 na wanaume asilimia 2.8.

Dk Marco amesema makadirio ya maambukizi ya UKIMWI kwa kila halmashauri hadi kufikia Desemba 2025  kwa  halmashauri ya Mji Ifakara imeongoza kuwa na asilimia tano na Manispaa ya Morogoro asilimia 4.4.

Amesema  Halmashauri ya wilaya ya  Gairo ina maambukizi asilimia 1.5, Kilosa asilimia 3.2 , Malinyi asilimia 2, Mlimba asilimia 3.3, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro asilimia 2.6 na Mvomero asilimia 2.1

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dk Adam Mrisho amesema kwa sasa maambukizi yamejikita kwenye watu wenye  umri  kuanzia miaka 15, 24 hadi 29 .

Dk Mrisho amesema watu hao wanapatikana maeneo mbalimbali, hivyo mkakati umewekwa kutolewa elimu kwa wanafunzi vyuoni , eneo la madini, uvuvi  na njia za masafa marefu.

Habari Zifananazo

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button