Wahamasishwa kuchangamkia fursa mfumo wa NeST

KIZAZI cha Samia maarufu ‘Generation Samia imewahamasisha wakazi wa mkoa wa Kanda ya Ziwa kuchangamkia fursa ya bajeti ya asilimia 30 ya tenda za serikali iliyotolewa makundi ya vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu kupitia mfumo wa NeST.

Kwa kutambua kuwa vijana ni chachu ya mabadiliko, Generation Samia imewasihi kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo, kwa kusajili vikundi vyao na kufuata taratibu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wamejisajili kwenye Mfumo wa NeST ili wajiinue kiuchumi.

Mikataba ya zaidi ya Sh trilioni 14.9 zimetolewa kwa wazabuni kupitia mfumo wa NeST, na mabilioni yametengwa kwa ajili ya makundi maalum, kwa mujibu wa PPRA.

Generation Samia kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) watafanya Kongamano la Wazi la Fursa za Kiuchumi, litakalofanyika Machi 29, 2025, Kwa Tunza Beach, Mwanza kuanzia saa mbili asubuhi. Kongamano hilo limebeba ujumbe, “Mgao wa 30% za Samia kupitia Mfumo wa NeST”.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button