Waiomba serikali usaidizi mauaji ya albino

SHIRIKA la Kimataifa lisilo la Kiserikali linalotetea haki za watu wenye ualbino ‘Under the Same Sun’ limesisitiza kuwa maendeleo mengi yaliyopatikana katika kusaidia watu ualbino yamesukumwa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.

Shirika limeeleza kuwa ni wakati wa Serikali kutoa msaada na msukumo katika kuthibiti mauaji kwani mashirika hayo pekee hayawezi kukidhi mahitaji .

Kwa mujibu wa Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika shirika hilo, Peter Ash amesema shirika limesisitiza licha ya juhudi zao, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali pekee  hayawezi kukidhi mahitaji ya watu 74,000 wenye ualbino nchini.

Ash alisema shirika lake nchini limefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 17 na kufunguliwa kwa kesi katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Vituo Vitatu vya Haki za Binadamu cha Chuo Kikuu cha Pretoria cha Afrika Kusini,Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo Afrika(IHRDA) na kusikilizwa kwa siku mbili yaani septemba 9 na 10 mwaka huu.

Maamuzi  yalitolewa mwishoni mwa mwaka huu ni hatua muhimu kwa watu wenye ualbino Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa mashambulizi ya kikatili dhidi ya watu wenye ualbino yanaendelea nchini na kesi mpya zikiendelea kujitokeza na hata katika miezi ya hivi karibuni mauaji ya kutisha ya mtoto wa miaka miwili Asimwe Novart yaliyotokea wilayani Muleba mkoani Kagera mapema mei mwaka huu ni ubaguzi wa msingi unaochochea mashambulizi hayo haujaondolewa.

Ash aliongeza kuwa kesi hiyo iishawishi Serikali ya Tanzania kuchukua hatua za kutekeleza mpango wa Kitaifa wa Ualbino ambao umekaa bila kutekelezwa kwa karibu miaka mitano kwani ni wakati dhabiti za kinga dhidi ya watu wenye ualbino Tanzania.

Naye Meneja Mratibu wa Village Of Hope ya jijink Mwanza Shirika linashughulika na Albino,Grace Wabanhu alisema kuwa ni wakati wa serikali kuwa na mpango wa Kitaifa wa kushughulikia changamoto za albino na sio kutoa na matamko ya kisiasa ambayo hayapo kwenye mpango wa kiserikali.

Wakati huo huo katika usikilizwaji wa kesi hiyo,Wakili wa Serikali Mkuu na Mkurugenzi Msaidizi wa Mashauri ya Kikatiba, Haki za Binadamu na Uchaguzi katika ofisi ya Wakili Mkuu wa serikali ,Hangi Chang’a alidai mahakamani hapo kuwa Serikali imekuwa ikishirikiana na Mashirika yasiyo ya kiserikali katika kutatua changamoto za watu wenye ulemavu wa Ngozi albino ikiwa ni poamja na kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika katika kuwauwa na kuwanyanyapaa.

Chang’a alidai hayo mbele ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu wakati ajibu hoja zilizowasilishwa na waleta maombi Mashirika manne yasiyo ya kiserikali mbele ya Majaji kumi wakiongozwa Makamu wa Rais Mahakama hiyo, Jaji Modibo Sacko.

Katika shauri hilo namba 016 la mwaka 2018,Wakili wa serikali Chang’a alidai kuwa kesi nyingi za albino zimekuwa zikishughulikiwa na Serikali ikiwa ni Pamoja na wenye kutenda matukio ya mauaji kufikishwa katika vyombo vya sheria na hatua kuchukuliwa.

Akiwasilisha maombi katika Mahakama mleta maombi wakili,Fulgence Masawe kutoka Kituo cha Haki za Binadamu alidai matukio mengi ya mauaji ya albino yamekuwa yakijirudia mfano kule katoro Geita na Kagera na kudai serikali kutoyachukulia kwa uzito mkubwa kwa kuwa yapo mashauri yaliyoenda Mahakamani lakini hayakupelelezwa vizuri.

Habari Zifananazo

Back to top button