WAJUMBE wa Bunge la Afrika (PAP) wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuondoa vikwazo vya biashara kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika kufikia eneo la Biashara Huru Bara la Afrika (AfCFTA) .
Pongezi hizo zilitolewa na wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na Profesa ,Margaret Kamar ambaye ni kiongozi wa ujumbe wa bunge la PAP wakati walipotembela Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani (OSBP) eneo la Namanga wilayani Longido mkoani Arusha.
Profesa Kamar amesema katika ziara hiyo wamefika nchini Tanzania kujionea jinsi ya utoaji wa huduma katika maeneo mbalimbali ya mipakani na kwa upande wa mpaka wa Namanga wamejionea jinsi nchi ya Tanzania inavyojitahidi kuhakikisha suala la usalama mipakani linaimarika ikiwemo utoaji na uingizwaji wa mizigo kupitia mashine zakisasa za ukaguzi.
Amesema ajenda kubwa ya mabunge hayo ni kuhakikisha biashara huru zinaimarika maeneo ya mipakani na wamejionea kwa macho yao juu ya biashara hizo na hatua zinazostahili katika ukaguzi mzuri unaofanywa katika eneo hilo la mpaka wa Namanga.
“Tumekuja kujionea jinsi gani nchi ya Tanzania inavyotekeleza fursa za biashara katika wa bidhaa zinazotokea nchi za EAC ikiwemo udhibiti wa bidhaa na uingizwaji lakini pia eneo la biashara huru lipoje tumeridhika na utaoji huduma nzuri katika maeneo ya mipaka hususan mpaka huu na wa Namanga unaounganisha nchi ya Kenya na nyinginezo.