Waishukuru taasisi ya Korea kusaidia huduma za afya

TAASISI ya kimataifa ya afya ya nchini Korea, imetoa jumla ya Dola za kimarekeni milioni tano, katika awamu ya pili ya mradi wa mapambano  dhidi ya vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga katika  halmashuri tisa za Mkoa wa Pwani.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Subira Mumba,wakati wa mkutano kutathimini miaka saba ya awamu ya kwanza ya mradi huo,  uliofanyika katika ukumbi wa shule ya kimataifa ya uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere mjini Kibaha.

Amesema fedha hizo ambazo zimetolewa kwa ufadhili wa taasisi hiyo  utadumu kwa miaka mitano na umelenga kuwafikia wanawake wote wajawazito, watoto wachanga wa Mkoa wa Pwani kupitia halmashuri tisa.

Advertisement

“Baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya mradi huu, tunaishukuru taasisi ya KOFIH kwa kukubali tena kutoa fedha zaidi ya Dola milioni tano za kimarekeni, ambapo kwa sasa wanawake na watoto wachanga wote wa mkoa wa Pwani watanufaika,”amesema.

Amefafanua kuwa awamu ya kwanza ya mradi huo, ilizinufaisha halmashuri za wilaya sita, ambapo uliwezesha kununulia magari matano ya kubebea wagonjwa, kujengwa kwa wodi za wazazi, ujenzi wa vyumba vya upasuaji katika vituo vya afya.

Alisema mradi wa awamu ya kwanza ulinza mwaka 2016 na kwamba umefanikiwa kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka watoto zaidi ya 800 na kufikia watoto 335, huku vifo vya wanawake vikipungua kutoka vifo 88 Hadi vifo 35.

Awali akizungumza katika mkutano huo kwa njia ya mtandao, Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya mama na mtoto, Wizara ya Afya, Dk.Ahmad Makuwani, alisema mradi wa kwanza uligharimu jumla ya Sh bilioni 9.5.

” Mradi huo wa awamu ya kwanza ulivifikia vituo vya afya 19 katika wilaya sita Kibaha Mjini, Kibaha Vijijini, Rufiji, Kibiti na Mafia ambapo ulijenga jengo la wazazi, vyumba vya upasuaji na vifaa tiba,” alisema

1 comments

Comments are closed.

/* */