Wajadili ushiriki wa wanawake katika siasa

SHIRIKA la Omuka Hub kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Marekani National Democratic Institute – NDI wameandaa majadiliano ya jukwaa la wanawake katika siasa kujadili mapendekezo ya kikosi kazi na maazimio ya Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama Vya Siasa yaliyotangazwa 13 Septemba mwaka huu.

Mjadala juu ya ushiriki wa wanawake katika siasa katika ngazi zote kuanzia kitongoji hadi taifa umefanyika Bukoba Mjini na kuhudhuriwa na washiriki 100 kutoka makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo viongozi wa dini, wanawake viongozi , wakuu wa mashirika/NGOs, viongozi wa kisiasa kutoka vyama vya siasa mbalimbali mkoani Kagera kwa lengo la kutoa maoni ambayo yatafanyiwa kazi na kikosi kazi.

Maazimio ya mjadala yanakwenda kuwa chachu katika utekelezaji wa maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha uwakilishi wa wanawake katika siasa.

Maazimio haya yatawasilishwa kwa kikosi kazi na msajili msaidizi wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza ambaye alisema mpaka sasa takwimu zinaonyesha kuwa ushiriki wa wanawake katika majukwaa ya kisiasa bado upo chini ambapo mwaka 2019 wenyeviti wa vijiji wanaume ni 11,915 wanawake ni 246 sawa na asilimia 2.1,Wenyeviti wa mitaa wanaume ni 4,171 na wanawake ni 528.

Alisema kuwa wenyeviti wa vitongoni wanaume ni 62,612 na wanawake ni 528 huku akisema kuwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa wanawake wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali.

Washiriki wa semina wamempongeza Rais Samia kwa hotuba nzuri aliyotoa wakati anafungua Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama Vya Siasa kwani hotuba inaeleza uhalisia na inatoa dira jinsi ambavyo shughuli za siasa zinapaswa kufanyika nchini.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
RosaPereira
RosaPereira
10 days ago

I am now making more than 350https://s.w.org/images/core/emoji/14.0.0/svg/1f4b0.svg dollars per day by working online from home without investing any money.Join this link posting job now and start earning without investing or selling anything……. 
🙂 AND GOOD LUCK.:)..____ http://Www.Careers12.com

Last edited 10 days ago by RosaPereira
Julia
Julia
10 days ago

I’ve got my first check for a total of 23,000 dollars. I am so energized, this is whenever I first really acquired something. I will work much harder now and I can hardly hang tight for the following week installment.
.
.
Detail Here………………………………………………………………… http://Www.BizWork1.Com

MONEY@
MONEY@
8 days ago

PATA DOLLA $45,000,000 SASA FANYA KAZI NYUMBANI NA HUTAKIWI KUTOKA HATA KIDOGO KABISA

TANGAzo

Chama cha MAPINDUZI kinawatangazia VIJANA WA KITANZANIA 500,000 kuandaa kijiji cha ujamaa eneo la UVUMI DODOMA…

WAHI FURSA HII ADIMU KWA MAENDELEO YA KARNE YA 23

Capture.JPG
Bima Ninayo
Bima Ninayo
8 days ago

IKASAIDIE KUONGEZA NGUVU ZA KIUME KWENYE VIJIJI VYA UJAMAA 

CaptureA.JPG
Back to top button
4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x