Wakandarasi wa ndani washindwe wenyewe sasa

DAR ES SALAAM: SERIKALI imeongeza wigo mpana katika sheria ya manunuzi ili kutambua wakandarasi wa ndani.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, jijini Dar es Salaam katika ugawaji wa tuzo za ujenzi na majengo Afrika Mashariki kwa mwaka 2023 (EABC).

Amesema, serikali itaendelea kuwaamini Wakandarasi wa ndani kwa miradi mbalimbali ikiwemo ile mikubwa ambayo wanaweza wakafanya vizuri kwani Serikali tayari imeongeza wigo mpana katika sheria ya manunuzi kwa lengo la kuwanufaisha Wazawa.

Hayo ameyasema wakati wa Ugawaji wa Tuzo za Ujenzi na Majengo Afrika Mashariki kwa Mwaka 2023 (EABC), zilizofanyika Katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Kasekenya amesema wahandisi wanapaswa wapate vifaa bora ikiwemo saruji, nondo, misumari, vigae, marumaru na bidhaa zote zinazotumika kwenye ujenzi ambazo zinazalishwa na kampuni hizo.

“Ukiwa mhandisi mzuri halafu ukapata bidhaa zisizo bora basi hautafanya chochote kizuri. Moja ya kitu ambacho Serikali tunakitaka ni kuwa na vifaa na uhandisi bora hivyo tunatoa wito kwa wadau wanaojihusisha eneo hili kutoa huduma zilizobora ambazo zinaingia kwenye mnyororo mzima wa ujenzi,”, amesema

Aidha, amewataka watanzania kuzidi kuwatumia wataalamu wa ujenzi pindi wanapokuwa na miradi ili kuwa na uhakika na usalama wa miradi yao kumalizika kwa wakati na kuwa bora.

“Usipowatumia wataalamu ujue mbele ya safari inawezekana ukapata hasara kama unajenga nyumba hakikisha imesanifiwa na mtaalamu hata asipojenga yeye hakikisha anakupa ushauriā€¯, amesisitiza Kasekenya

Tuzo za Ujenzi na Majengo za Afrika Mashariki kwa Mwaka 2023 umeshindanisha makampuni zaidi ya 500 kwa lengo la kuongeza ushindani miongoni mwa wadau wa Sekta ya Ujenzi, lakini pia kufanya chachu ya utoaji wa huduma bora katika mnyororo mzima wa Sekta ya Ujenzi.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button