Wakandarasi wazawa kukuzwa kimataifa

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa ametangaza mkakati wa kukuza na kuendeleza wakandarasi wazawa ili wafikie viwango vya kimataifa vya ubora na usalama.

Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa kikao na watumishi wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kilichofanyika makao makuu ya TARURA jijini Dodoma.

Amesema Serikali imejipanga vyema kuhakikisha inawanyanyua wakandarasi wazawa na kusisitiza kuwa pamoja na majukumu ya TATURA pia wana jukumu la kukuza na kuwaendeleza wakandarasi wazawa.

“Hatuwezi kuitenganisha TARURA na wakandarasi wa ndani kama ambavyo huwezi kuitenganisha TAMISEMI na wananchi, maendeleo ya miundombinu yanamchango katika uchumi wa wananchi na wa Taifa.”

“Mikakati ya TARURA ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 tuwe tumeboresha barabara za vijijini na mijini kwa asilimia 85 lakini tukiwa tunaenda kuyafikia mafanikio hayo lazima tujiulize tumewakuza na kuwajenga wakandarasi wangapi wazawa?

Tumewanyanyua kiasi gani kufikia viwango vya kuwafanya washindane kimataifa.”
” Kwa hiyo ninawataka, pamoja na majukumu mengi mliyonayo TARURA kwenye uongozi wangu kama Waziri jukumu la kukuza na kuwaendeleza wakandarasi wazawa nitalipa kipaumbele cha hali ya juu. Na leo natangaza rasmi mkakati wa kukuza wakndarasi wazawa utakaosimamiwa na ninyi TARURA.”

” Nitawapa TARURA mnisaidie ili tunakokwenda tuwe tumewajenga wakandarasi alteast kila mkoa kampuni za wakandarasi 20 tutakua kumekuza Kampuni za Wakandarasi takribani 520 katika mikoa yetu yote 26.”

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
haunameno
haunameno
1 month ago

Wahi Viwanja Vya Bure Ulichopewa na Nyerere wakati wa Uhuru… Kina sifa ya kuwa kidogo na STORY ZA R.I.P NA “INA ILAH LAJUUN”. – HAKIKA ALIKUDHAMINI SANA

Capture.JPG
haunameno
haunameno
1 month ago

Wahi Viwanja Vya Bure Ulichopewa na Nyerere wakati wa Uhuru… Kina sifa ya kuwa kidogo na STORY ZA R.I.P NA “INA ILAH LAJUUN”. – HAKIKA ALIKUDHAMINI SANA..

Capture.JPG
Marry
Marry
1 month ago

I’m currently generating over $35,100 a month thanks to one small internet job, therefore I really like your work! I am aware that with a beginning capital of $28,800, you are presently making a sizeable quantity of money online.
.
.
Just open the link——->> http://Www.Smartcareer1.com

Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x