Wakili Revocatus Rutta ajitosa Iringa Mjini

IRINGA: Wakili Revocatus Rutta amejiunga rasmi katika orodha ya wagombea wanaowania kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini.
Rutta amejiunga na orodha ya waliokwisha kuchukua fomu akiwemo Fadhili Ngajilo, Mchungaji Peter Msigwa, Wakili Moses Ambindilwe, Nguvu Chengula, Ally Msigwa, na Islam Huwel.
Mwingine anayesubiriwa katika mchakato huo ni mbunge anayemaliza muda wake, Dk Jesca Msambatavangu.



