Ujerumani kuwapokea wakimbizi 942

BERLIN, UJERUMANI: SERIKALI ya Ujerumani imesema imewapokea wakimbizi 942 kutoka nchi mbalimbali duniani kwa mwaka huu kupitia mpango wa Umoja wa Ulaya wa kuwapatia makaazi mapya.
Wakimbizi hao wanatoka Sudan, Syria, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Eritrea na mataifa mengine. Hata hivyo, tangu serikali mpya iingie madarakani Mei 7 mwaka huu, hakuna wakimbizi zaidi waliopokelewa nchini humo.
Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, makubaliano ya serikali ya muungano wa vyama vya CDU/CSU na SPD yanataka programu za kuwasaidia watu kutoka maeneo ya mizozo kusitishwa, huku zikiwa hazitazinduliwa tena mipango mipya.
Chini ya mpango wa Umoja wa Ulaya, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) hutambua watu walio hatarini kabla ya kuwapatia makaazi mapya. Baadaye mamlaka za Ujerumani hufanya mahojiano na ukaguzi wa usalama. SOMA: Msumbiji yakumbwa ongezeko la wakimbizi