DAR ES SALAAM: WAKRISTO wametakiwa wamwambie Mungu ahsante kwa zawadi ya Yesu Kristo kuja ulimwenguni na kuukomboa ulimwengu na ameleta amani.
Hayo yamelezwa leo na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Dk, Titus Mkama katika maadhimisho ya Sikukuu za Krismasi alipohubiri katika Kanisa hilo Ilala Dar es Salaam.
Vilevile amewataka wakristo na wasiyo wakristo wasishi gizani na badala yake waitafute nuru kuu na si nuru nyingine bali ni Yesu Kristo na ili uipate nuru hiyo hawanabudi kumkiri Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa Maisha yako.
“Ulikuwa ni mtu wakuangamia lakini nuru imekumulikia njia ya furaha, amani na matumaini na ukitembea ndani ya nuru hiyo Maisha yako yatakuwa tofauti na utabarikiwa mno na amezidisha furaha ndani yako, siku kama ya leo siyo yakuchukulia kirahisi inakupasa ukae na utafakari ulikotoka, ulipo leo, na wapi unakoelekea” alisema
Aidha aliwataka wakristo kuikataa dhambi maana kwa ajili yetu amezaliwa mtoto mwanaume na uweza wakifalme utakuwa begani mwake kwa ajili ya wanadamu.
“Leo ukienda Muhimbili watu wanatoa hongera kwa mama aliyejifungua na wanaingia kwa miyoyo ya furaha na wewe lazima ufurahi ni kwa ajili yako na siyo ya fulani na awe kwa ajili yako wewe mwenyewe binafsi amezaliwa mtoto mwanaume huyu mtoto ni watofauti ana uweza wa kifalme na kiutala, ana uweza wakusababisha amani duniani kote huyu ni mtoto wa ajabu tuliyepwa ni zawadi kubwa kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu mwenyezi ukae salama na usalama upo kwa Yesu Kristo mwokozi” alisema Mkama
Mchungaji Mkama alitoa sifa za Yesu Kristo kwamba ni mshauri wa ajabu ana uweza wakumshauri mtu asiyekuwa na amani hadi awe na amani, anayekwenda gizani atamrudisha nuruni,wapo wanaosomea Saikolojia lakini hawana uweza wakushauri watu ndiyo mana kuna wavutabangi, walevi na wahuni.
“Ndiyo maana watu wanauana mke anaua mume na mume anaua mke ni kwa sababu wamemkataa Yesu, akikushauri utajisikia furaha maana umekutana na mshauri wa ajabu na pia ni Mungu mwenye nguvu na hashindwi na jambo ana nguvu hakuna linalomshinda kwakuwa amepewa ufalme na nguvu na ni baba wa milele” alisema Mchungaji Mkama
Comments are closed.